Kipindi rais Magufuli ameingia madarakani, watanzania walikuwa wanampenda na kumuelewa sana, hata wale ambao hawakumpigia kura walijilaumu sana.
Lakini sasa hali imekuwa tofauti, amekuwa rais ambae anachukiwa sana na wananchi wake, ukitembea maeneo mbalimbali watu hawataki hata kusikia jina lake, wale waliokuwa wanamsifia wamegeuka na kuanza kuponda utawala wake.
Zipo sababu nyingi lakini moja ni hulka ya rais wetu kuweka tabia yake binafsi kwenye uongozi, rais kuonesha hawajali watanzania wenzake na hata wanapolia anawatolea maneno ya kejeli na dhihaka.
Watu wanalalamika na hali mbaya ya uchumi, pesa mtaani haionekani lakini rais amekuwa kimya, hajali, na baadala yake anawaita wapiga dili, fikria usumbufu wanaokumbana nao wafanyabiashara toka kwa maafsa wa Tra, kubambikiwa kodi kubwa, kuambiwa wawe na mashine za EFD ili hali mitaji ni midogo, mtu ana mtaji wa million 1 anaambiwa awe na mashine ya EFD ya Tsh 800,000/=kwanini mtu huyo asiuchukie utawala huu.
Wapo vijana wamehitimu vyuo vikuu hawana kazi, mfano kuna uhaba mkubwa sana wa wahudumu wa afya kama manesi na madaktari, lakini wapo vijana wengi wamehitimu na wapo nyumbani wamekaa.
Watumishi wa umma ni mwaka wa 3 hakuna nyongeza wala madaraja, kuna watu wanapokea mishahara midogo sana kutokana na ongezeko la makato la HESLB.
Kuna matukio ya kinyanyasaji wanayofanyiwa viongozi wa vyama vya siasa, ikiwemo utekaji, uteswaji, kupigwa risasi hadharani lakini pia tumeona ubakaji wa wazi wa demokrasia kwenye chaguzi ndogo.
Rais anafanya upendeleo wa wazi kwa watu wa kabila Lake, teuzi nyingi zinaegemea huko, huko wananchi wakivunja sheria na kuvamia maeneo ya serikali wanaachwa kwa sababu wamemchagua ili hali wananchi wa upande mwingine wamevunjiwa nyumba zao.
Ukweli ni kwamba watanzania ni waelewa sana na hakuna mtu anaeweza kuwafitinisha na viongozi wao, chuki mbaya kwa utawala huo ni kutokana na matendo ya viongozi hasa kiongozi mkuu, tuache kuwasingizia wapinzani.