Tuseme kuwa Jk atakuwa mtawala wa Tz. kwa kipindi cha 2010-2015.
Nimetambua kuwa Tanzania tunajihangaisha kufanya uchaguzi ili kupata viongozi kumbe Tanzania hatuna viongozi bali Watawala. Hali hii siwezi kukubaliana nayo kabisa. Lazima tuwe na fikra pevu kwani haiwezi kuingia akilini mtu anayeomba nafasi ya uongozi ndiye huyo huyo anayeagiza NEC watanzaze kile anachotaka yeye. Tuambiane ukweli, hata kama JK hajachaguliwa na wananchi Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi atamtangaza mtu mwingine ambaye siyo JK? Makame (Mwenyekiti wa Tume) anawajibika kwa JK kwa utaratibu wa kazi, je makame atakuwa anapokea maagizo toka kwa nani? Kama ni kutoka kwa Jk, ni aina gani ya maagizo kama siyo kwamba Jk atangazwe mshindi?
Tunapotaka tuiamini Tume ya uchaguzi ni kwa misingi gani tuiamini, Tume gani inayowajibika kwa yule yule ambaye ana maslahi anayoyataka kutoka kwa Tume hiyo hiyo. Ndiyo maana moja ya mambo mazito ambayo Dr. Slaa alitaka yafanyiwe kazi baada ya kuchaguliwa ni marekebisho ya katiba.
Kwa mwenendo huu Watanzania tunachezewa akili, tunaporwa haki zetu. Tutambue kuwa sasa tumeanza kutawaliwa na kama hatutaki kutawaliwa lazima tuchukue hatua. Haki haiombwi bali inadaiwa. Kura zetu za kuchagua viongozi wetu lazima zifanye kazi iliyokusudiwa isiwe kibali cha kuwaweka watawala madarakani kwa kuundiwa usanii wa Tume ya Uchaguzi na vyombo vingine kama TAKUKURU. Tangu uchaguzi ulipoanza TAKUKURU walienda likizo huku CCM wanagawa kanga, kofia, fedha nk. Baada ya kuona hilo nalo halijasaidia wakaagiza Wasimamizi wachakachue matokeo ya kura. Tuamke Watanzania, hali hii haipaswi kuachwa hivi hivi