Utawala wa Jk 2010-2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utawala wa Jk 2010-2015

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Gurtu, Nov 4, 2010.

 1. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #1
  Nov 4, 2010
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Tuseme kuwa Jk atakuwa mtawala wa Tz. kwa kipindi cha 2010-2015.

  Nimetambua kuwa Tanzania tunajihangaisha kufanya uchaguzi ili kupata viongozi kumbe Tanzania hatuna viongozi bali Watawala. Hali hii siwezi kukubaliana nayo kabisa. Lazima tuwe na fikra pevu kwani haiwezi kuingia akilini mtu anayeomba nafasi ya uongozi ndiye huyo huyo anayeagiza NEC watanzaze kile anachotaka yeye. Tuambiane ukweli, hata kama JK hajachaguliwa na wananchi Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi atamtangaza mtu mwingine ambaye siyo JK? Makame (Mwenyekiti wa Tume) anawajibika kwa JK kwa utaratibu wa kazi, je makame atakuwa anapokea maagizo toka kwa nani? Kama ni kutoka kwa Jk, ni aina gani ya maagizo kama siyo kwamba Jk atangazwe mshindi?

  Tunapotaka tuiamini Tume ya uchaguzi ni kwa misingi gani tuiamini, Tume gani inayowajibika kwa yule yule ambaye ana maslahi anayoyataka kutoka kwa Tume hiyo hiyo. Ndiyo maana moja ya mambo mazito ambayo Dr. Slaa alitaka yafanyiwe kazi baada ya kuchaguliwa ni marekebisho ya katiba.

  Kwa mwenendo huu Watanzania tunachezewa akili, tunaporwa haki zetu. Tutambue kuwa sasa tumeanza kutawaliwa na kama hatutaki kutawaliwa lazima tuchukue hatua. Haki haiombwi bali inadaiwa. Kura zetu za kuchagua viongozi wetu lazima zifanye kazi iliyokusudiwa isiwe kibali cha kuwaweka watawala madarakani kwa kuundiwa usanii wa Tume ya Uchaguzi na vyombo vingine kama TAKUKURU. Tangu uchaguzi ulipoanza TAKUKURU walienda likizo huku CCM wanagawa kanga, kofia, fedha nk. Baada ya kuona hilo nalo halijasaidia wakaagiza Wasimamizi wachakachue matokeo ya kura. Tuamke Watanzania, hali hii haipaswi kuachwa hivi hivi
   
 2. SUNGUSIA

  SUNGUSIA JF-Expert Member

  #2
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 232
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  naunga mkono hoja asilimia 200, we need change kubwa sana hasa kwenye KATIBA yetu, haya yote yanayo endelea ni kwasababu katiba yetu inatoa mianya hiyo.
   
 3. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #3
  Nov 4, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  mwishoni mwa utawala wa kikwete 2015 tutegemee yafuatayo..

  1. mfumuko wa bei 50%

  2.exchange rate at Tshs 3500/= per 1USD


  3. lita moja ya petroli at Tshs 3300/=
   
 4. M

  MpitaNjia Member

  #4
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh kaaaaaaaaaazi kweli kweli hapo WATANZANIA wengi watakufa kwa BP...........
   
 5. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #5
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Sheria ndiyo inayo muongoza na wala sio JK. Km mwataka tofauti badilisheni sheria na sehemu yake ni bungeni . Si tundu lissu yupo , mpeni hoja hiyo aipeleke .
   
 6. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #6
  Nov 4, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  On a seriuos note hakuna haja ya kufanya uchaguzi kama mshindi anajulikana
   
 7. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #7
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Naombeni wana forum mniambie ni nani mngetaka awe Mwenyekiti wa tume? Kama hawakuwa na imani mbona hawakusema toka mwanzo?

  Najua yule mzee ni muungwana angejiuzulu halafu apatikane mtu mwengine.

  Nani atoe haki zaidi ya Judge?
   
 8. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #8
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,728
  Likes Received: 1,636
  Trophy Points: 280
  eti uchumi umekua kuna magari mengi kila nyumba mzuri kuna gari zaidi ya moja yaani ya baba na mama na watoto ati, sijui hayo magari watweka mafuta gani na kama nikubadilisha mfumo wa gesi gesi yenyewe bei juu
   
 9. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #9
  Nov 4, 2010
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Bei ya Petrol hapa Arusha leo ni 1800 Tshs.!
   
 10. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #10
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Na hivi mmechagua Lema mtakoma safari hiii, adhabu yenu inakuja !
   
 11. jcb

  jcb JF-Expert Member

  #11
  Nov 4, 2010
  Joined: Jul 6, 2010
  Messages: 281
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nimeipenda sana hii. Nimetafakari kuhusu hili tokea matokeo yalipo anza kutangazwa nakosa majibu ni kwa nini tuna poteza gharama nyingi na muda wetu kuelekea kwenye vituo vya kupigia kura wakati kuna watu wanakuwa wamepanga matokeo tayari.
  Hii ndiyo mara yangu ya mwisho kupiga kura haitatokea tena!!!!!!!!!!!!!!!!!! :A S angry:
   
 12. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #12
  Nov 4, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Na wananchi wamedanganywa kwa shs. 5000, fulana, kofoa ma kanga. How long will these last. One thing I am certain of ni kuwa umasikini utaongezeka ukiambatana na ongezeko la ufisadi, umwinyi na usultani in the likes of Ridhiwani, January etc etc. Kila mara namkumbuka Mwl. Nyerere aliposema wakati anaugua kuwa anawasikitikia sana Watanzania wake.

  Uchaguzi ukiisha napanda ndege kwenda kupumzika elsewhere na nitakuwa niki post humu from there for the next 5 years.
   
 13. n

  nkosiyamakosini Member

  #13
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi kuna sheikh yahaya humu ndani? naona twatabiri bei za petroli 2015! kaaz kwelkwel. thanks
   
 14. October

  October JF-Expert Member

  #14
  Nov 4, 2010
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 2,147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nakubaliana na wewe 100%. Hakuna haja ya kutumia gharama kama zilizotumika kugharamia uchaguzi kama hakuna utashi wa kisiasa wa kuwa na uchaguzi. Ni afadhani itangazwe rasmi kuwa Tanzania ni nchi ya chama kimoja tujue kuliko kuwafanya watu watoto.
   
 15. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #15
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  tanzania bila ccm haiwezekani !!!!!!!!!
   
Loading...