Utawala Bora Tanzania,zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utawala Bora Tanzania,zanzibar

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by GHIBUU, May 24, 2011.

 1. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #1
  May 24, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  [​IMG] Siku hizi, wataalamu wengi wanazungumzia dhana ya utawala bora. Imekwua midomo haipumziki, bila kuitaja ‘utawala bora’. Lakini, kusema kitu chengine na kufanya jambo nyengine kabisa. Aghlabu, dhana hii, kwa nchi kama zetu, huambatana na watendaji wa serikali husika, na pesa, kupata pesa za wafadhili tu. Basi.
  Sasa angalieni utawala bora Zanzibar:
  1. Jaji ametoa hukumu ya kuwa wenye makontena pale Darajani, waruhusiwe kufanya shughuli zao, na makontena yafunguliwe. Baraza la Mji wa Zanzibar limekataa mari ya mahkama. Kwa ufupi, hukumu,imetolewa kuwa rukhsa kuendelea kufanya biashara hapo. Just mtu mmoja wa Baraz ala Mji amepinga amri hiyo, kwa hisia zake za ukereketwa.
  2. Wasomi wetu wenye madigree kibao, awali, wameipeleka kesi ya wanaodaiwa kuchoma moto vibanda vya watoto wa waflme wetu kule Pwani Mchangani, isikilizwe mahkama kuu. What? Mahkama kuu ili kuwaridhia wabwana zetu. Kesi hii mimi niliyekuwa zuzu wa sheria, ninajua kuwa si kesi ya kwenda mahkama kuu — hii ni kesi ya district court au tuseme regional magistrate.
  Lakini, kwa vile tunataka kuwaridhia wafalme, lazima tuonekane kuwa ni jambo kubwa, tumevunja na kutia moto palace. Jana, kwa aibu, uamuzi mwengine umetolewa kuwa kesi ihamishiwe mahkama ya Mfenesini. Hivi kweli jaji aliyeichukua kesi hii tokea mwanzo hajui hili. Ina maana ni hatari wanasheria wetu, kuwa basic ya ABCD ya sheria hawaijui.
  Hiyo ndio faida ya kuweka watoto wetu ndani mfumo wa sheria. Lakini msisahu kuwa kuanzia mrafjis, mpaka muendesha kesi, anatoka huko huko Tanganyika, ni ama Abraham Mwanpashe au jaji…gani sijui. Tumewaleta wenyewe ili wawahukumu CUF (enzi zile) sasa wanatupanda juu ya kichwa. Bado….tutaona. Na tutazidi kuona. wazee wetu walisema ‘ukitaka nyingi nasaba, utapata mwingi msiba’.
  Hivi kweli mtu kama Abubakar Khamis Bakari, Waziri wa Sheria (kutoka CUF: Slogan — Hakiiiiii, hakuliona hili?) kama hakuliona hafai – na ajiuzulu. Udhaifu wa kujua kazi, au vacuum kama jiyo, ndio anakuja Dr.Bilali anasema vile anavyoona yeye kuwa sasa ardhi ya watu wazawa, wapewe jamaa zake wa Kijaluo, na Kimasai n.k. Jamani mtu kwao, Dr.Bilali Mjaluo wa Uganda, lazima atavutia watu wake waje hapa Zanzibar. Watu tusiokuwa na hisia nzuri za kwetu ni sisi wazanzibari tu, tunatiana visu vya roho wenyewe kwa wenyewe.
  Hili jengine si letu. Lakini nitalisema. Mauwaji ya Raia Tarime. Ploisi imeuwa, lakini hakuna aliyesmea kuwa kuna ukiukwaji wa haki za binadamu Tanzania. Nilidhani kuwa serikali itawatia mbaroni waliouwa na kushtakiwa. Leo, wanalaumiwa ‘maiti’ kuwa wao ndio chanzo cha vurugu, an Chadema….iwe ndio hivyo, lakini hakuna justification ya kuuwa. Heko Utawala Bora TZ.
  Gumzo la mji leo hapa mjini na vitongoji vyake, ni kuhusu kesi ya Pwanimchangani. Ni aibu kwa mahkama, ni aibu kwa wanasheria, ni aibu kwa utendaji mzima wa SMZ-GNU. Ni aibu hata kwa mtu kama Maalim Seif ambaye alisimamia slogan ya HAKI huko nyuma, sasa amebaki kuzungumzia ‘maharamia wa kisomali tu’. Labda sasa tumpangie kazi katika department ya CIA ya ‘counter-terrorism’ aende kumsaka Al-Zawahir, Mullah Omar, n.k
   
Loading...