Utawaambiaje Bodaboda Lowassa kashindwa wakuelewe?

Utawaambiaje Bodaboda Lowassa kashindwa wakuelewe?

Mkurabitambo

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2010
Posts
230
Reaction score
57
Habarini,

Kama mjuavyo asilimia 57 ya wapiga kura ni vijana ambao kwa hesabu za haraka 50% watampigia kura Lowassa na hao 7% hawaeleweki. Ili kupata ushindi Rais anatakiwa awe na kura zaidi ya 50%, kwa kuangalia orodha ya Tume inaonesha wengi ni wapiga kura wa Lowassa, wanatarajia Lowassa ashinde.

Bado nawaza, hasa kuhusu Bodaboda ambao hata ukimgusa mmoja na gari wanakufuata watu 100 na hawanaga msalia mtume, utawaambiaje watu hawa wakuelewe eti yule wanayemwona kuwa ni mkombozi wao kashindwa urais.

Bado nawaza.
 
Hapo hamna namna Buldozer zipo za maji ya kuwasha. Akili za maccm
 
Watasaidiwa kueleweshwa!

Kweli watasaidiwa waelewe wakigoma wanapata kichapo cha mbwa mwizi. Unafikiri hapo ni kugonga gari la mtu binafsi??? Hapo ni usalama wa nchi na hakuna jinsi
 
Wataelewa wakiwa selo miguu vipande vipande.
 
Huyo atakae tangaza itabidi atangaze akiwa ndani ya gari ya police na baada ya hapo ajiandae kwenda ICC
 
Kwani CCM haina vijana? ama kwasababu unakoishi umejifungia kwenye vioo? kwahiyo kwenye vijiji na mijini mikutano ya Magufuri ilikuwa na wazee tu na watoto wa chekechea?
 
Kweli wewe gutumbo.....waendesha Bodaboda ni kaka na Dada zako tena ni watanzania kama wewe...

Kaka na dada ambao ni watanzania wenzetu sio watu wavurugu hao ambao mnawasifia humu eti matokeo yakitangazwa kams lowassa kashindwa hawataelewa.

Hakuna mtanzania ambaye ana akili mbovu na kukumbatia vurugu. Wao wana pikipiki sisi tuna magari walete huo uwendawazimu waone.
 
We Wee,akili Zako Finyu....Utawaelewesha Wewe Na Mbowe...
"magufuli Atosha Mamvi Yanini?"
 
Nafikiri wataelewa tu kwani wapo bodaboda wanaoiunga mkono ccm kwa baadh ya maeneo na usishangae maajabu ya dunia ukwaona wanashangilia tena kwa furaha, na kuna waajiri watazichukua pikipiki zao jumamosi kuhofia kuharibiwa na polisi wetu wasiokuwa na huruma, nimeshuhudia leo kuna baadhi wanaanza kurudisha pikipiki za watu.
 
Kwani CCM haina vijana? ama kwasababu unakoishi umejifungia kwenye vioo? kwahiyo kwenye vijiji na mijini mikutano ya Magufuri ilikuwa na wazee tu na watoto wa chekechea?

Yaani hapa nimemshangaa mleta mada kwenye kundi la vijana wapo pia vijana wa kike (wadada) . ambao ndio wengi je nao ni boda boda, vipi vijana waliopo vyama vingine. sikubaliani na takwimu ya kuonesha vijana ni wa kiume tu tena bodaboda
 
Kwani CCM haina vijana? ama kwasababu unakoishi umejifungia kwenye vioo? kwahiyo kwenye vijiji na mijini mikutano ya Magufuri ilikuwa na wazee tu na watoto wa chekechea?

Walikwenda kutazama fiesta..
 
kama nchi hii imefikia hatua ya kuogopa kusema ukweli kwa kuwaogopa bodaboda basi tukubali kuwa tumeiharibu nchi kwa mikono yetu wenyewe.
 
Nafikiri wataelewa tu kwani wapo bodaboda wanaoiunga mkono ccm kwa baadh ya maeneo na usishangae maajabu ya dunia ukwaona wanashangilia tena kwa furaha, na kuna waajiri watazichukua pikipiki zao jumamosi kuhofia kuharibiwa na polisi wetu wasiokuwa na huruma, nimeshuhudia leo kuna baadhi wanaanza kurudisha pikipiki za watu.

juzi limnyanganya wa kwangu mim nimepatia ajiri sasa nikamkuta amejaza mabendera ya chadema kwa kufuata mkumbo nikamwambia anikabidhi funguo zangu haraka sana amfuate BOSS WAKE kubenea
 
Na ndio nilichokiona, jamaa wanachukua pikipik zao na wanazifungia ndani kwani nyingi zitapigwa moto yani wakikunasa ni kibiriti tu sasa huyo mmiliki lazima akutie jela, na sioni madhara ya hawa watu labda tunajaribu kuwa boost tu ila nao watakuwa wapole kwasababu sio kila eneo lenye bodaboda ni ngome ya ukawa
 
Back
Top Bottom