Utaungaje bajeti mkono mia kwa mia?

Moony

JF-Expert Member
Apr 16, 2011
1,599
435
Jamani mie nashindwa kuelewa; mtu unaunga bajeti mkono mia kwa mia pamoja na utititiri wa malalamiko na ukosoaji wa bajeti.
Je hii ndiyo kanuni ama ndio utaratibu?
Ingebidi kila mbunge aliyelalamikia bajeti hata kipengele kimoja basi apunguze asilimia na kuwe na data. Inaelekea hata rekodi hamna bunge linapelekwa pelekwa tu na kuendeshwa kienyeji.

huwezi kulalama na kukosoa halafu ukatoa maksi 100%:embarrassed:
 
We unasema kunga mkono kwa 100%, mi nimemsikia mbunge wa CCM sasa hivi akiunga mkono bajeti kwa 500%.
 
upuuzi mtupu . huwezi kabisa kutofautisha mchango wa mbunge aliyesoma hadi akaitwa professor na mbunge a,baya kaishia Elimu ya Seondary . Kwa mtazamo wangu mtu akisema anaunga mkono kwa %100 au hizo 300% kama kweli ipo kimahesabu.
Kwa uelewa wangu mtu akiunga hoja kwa asilimia 100% sudhani kama atastahili kukosoa kama ambavyo nawasiia baadhi ya hawa wabunge wanaounga mkono hoja kwa %300 na kuanza kutoa malalamiko lukuki, Kuna baadhi ya watu watasema hayo sio malalamiko bali ni michango ya kuboresha bajeti.
Nadhani ingetungwa kanuni ya bunge kwamba wale wabunge wanaounga mkono hoja yeyote bungeni kwa %100 wasipewe nafasi kuchangia lolote manake wanaikubali hoja hiyo na so kuwaruhusu kuchangia ni sawa na kupoteza muda tu, wangeruhusiwa kuchangia ambao hawaungi mkono bajeti ili mawazo yao yaweze kuingizwa kwenye bajeti .
Mtu anaunga mkono kwa% 300 zen anaaza kutoa malalamiko mwanzo mwisho haiingii akilini kabisa
 
Back
Top Bottom