Utatu wa Dkt. Magufuli, Eng. Kijazi na Eng. Mfugale katika ujenzi wa barabara nchi nzima tutaukumbuka milele

Barabara ya Jet corner hadi Davis corner na ile ya kutoka Mbezi hadi Goba zote zilijengwa wakati wa Kikwete tafuteni barabara nyingine alizojenga sio kumpa sifa za mwingine.
Unachosahau Magu alikuwa Waziri wa ujenzi,Kijazi alikuwa katibu na Mfugale alikuwa mkurugenzi wa TANROADS
 
Utatu unaozungumzwa hapa ni: Waziri - Katibu mkuu - DG Tanroads

Utatu huu umeanza kujenga barabara awamu ya mzee wa Lupaso, Ben Mkapa!
Kama mtoa mada alikuwa na maana hiyo, kwanini hakutaja barabara nyingine au walijenga hizi tu?
 
Kweli kabisa, hizo barabara zilijengwa na Kikwete. Mzee Kikwete watu wamemu-underate sana. Kafanya mambo makubwa sana yule mzee nadhani ndio kiongozi bora kiutawala baada ya Mwalimu

Tuangalie sekta moja ya afya ambapo Muhimbili ilijengwa na mkoloni almost 50% ya majengo yaliyopo pale. Alikuja Mwalimu akaongeza baadhi machache, Ruksa hakufanya chochote, Mkapa alikarabati miundombinu iliyopo ila akuongeza.

JK alijenga JKCI, New OPD, MOI na Mloganzila

Kwenye barabara za mikoa JK ndiye aliyeunganisha nchi yote kwa barabara. Amejenga airport mpya, mradi wa mwendokasi, mradi wa ubungo flyover (alianza yeye) na mingine mipya. Through JK nchi iliingia uchumi wa kati wa chini.

Nitamkumbuka na kumuenzi daima JK na katika utawala wake ndipo hata maeneo mengi ya jiji yaliendelea baada ya watu kuwa njema kiuchumi kama Madale, Malamba Mawili, Goba, Bunju, Kigamboni, Mabwepande, Kongowe ya Dar, Chamanzi n.k
Ngoja team legacy waje 😂😂😂
 
Limekugonga utosini jiwe...Pole! Acha hasiara Tanzania ni ya watanzania siyo ya makundi fulani. Mwelewe Mh. Rais yeye hana hizo tabia kutwa kucha kumchonganisha kwasababu zenu binafsi!
Kwahiyo ndio kila kitu kizuri kilichofanywa hata kama kimefanywa na mtu mwingine bado mumsifie yeye na sisi wengine tunyamaze tu!
 
Eneo kubwa la barabara ulizosema zimejengwa kuanzia wakati hao wote wakiwa wizara ya Ujenzi.
Lini mmeanza kuwasifia mawaziri wa sekta husika, Mbona sijawahi kusikia mkimsifia waziri Mbarawa kuhusu ujenzi wa barabara zilizojengwa wakati Magufuli akiwa Rais? Acheni mambo yenu lengo lenu ni kumsifia Magufuli binafsi kwa kila kitu sema mkiumbuliwa mnatafuta pa kutokea.
 
Legacy yake itadumu milele, JPM hatunaye kimwili lakini ameacha ametengeneza akina JPM wengi Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Tutaenzi yote mazuri Kama hulka yake ya kusema ukweli na kutokuwa mnafiki, uwezo wa kufanya maamuzi na kuyasimamia bila kuyumba, uwezo wake wa kuchapa kazi usiku na mchana, uzalendo katika kusimamia rasimali za nchi na kupambana na ufisadi na rushwa.

Sent from my itel W6004 using JamiiForums mobile app
Mimi najua legacy yake kubwa ni roho mbaya na asiyependa kuona mwingine yupo juu yake yaani ni mtu mwenye roho ya kwanini.
 
Unachosahau Magu alikuwa Waziri wa ujenzi,Kijazi alikuwa katibu na Mfugale alikuwa mkurugenzi wa TANROADS
Kwahiyo,mbona sasa hivi amuwasifii hao mawaziri, makatibu wakuu na wakurugenzi au wakati Magufuli akiwa Rais yeye ndiye alikuwa waziri wa kila wizara yeye pia alikuwa katibu mkuu na mkurugenzi kila sehemu?
 
Nimepita kwa daladala kutoka Temeke - Lumo jet - Kinyerezi hadi Mbezi mwisho stendi ya mkoa lami tupu sijagusa vumbi.

Nikatoka Mbezi mwisho hadi Bunju kupitia Madale ni full mkeka no vumbi.

Kwa hakika Magufuli - Kijazi - Mfugale tutawakumbuka daima.

Raha ya milele uwape ee Bwana, Wastarehe kwa amani, amen!
Chato/Geita—Tanga—Iringa. Ndiyo uone Mzee alivyokuwa anafuata ushauri wa kitengo. Alikuwa haangalii eti msukuma mwenzangu au ndugu yangu.
 
Urais siyo kujenga barabara tu mkuu. Rais ni zaidi ya barabara labda unataka kutwambia kuwa jpm hakufaa kuwa rais bari waziri wa miundombinu tu.

Huwezi kuuwa, kupoteza watu na kukandamiza kila anauekupinga halafu eti barabara ndo zikuokoe. Bora limekufa tu sasa hivi tuanapumua na biashara zimerudi pia ajira sasa hivi ni choice la sivyo tulikuwa tunakufa kimyakimya
Ye katoa post baada ya mizunguko aliyoifanya. Kuna mwingine anaweza kuzungumzia umeme baada ya kuzunguka vijijini na kukuta umeme umetapakaa.
 
Lini mmeanza kuwasifia mawaziri wa sekta husika, Mbona sijawahi kusikia mkimsifia waziri Mbarawa kuhusu ujenzi wa barabara zilizojengwa wakati Magufuli akiwa Rais? Acheni mambo yenu lengo lenu ni kumsifia Magufuli binafsi kwa kila kitu sema mkiumbuliwa mnatafuta pa kutokea.
Mimi ni kati ya watu niliosikitika kuondoka kwa Prof. Muhongo wizara ya Nishati.

Nilimpondea sana Kalemani mwanzo wa uongozi wake wizara ya Nishati na kumsifia mtangulizi wake.

Na hapo kama umefuatilia mjadala hajasifiwa raisi pekee bali muunganiko wa raisi, waziri wa ujenzi na mkurugenzi wa TANROADS ingawa baadhi ya hizo barabara zilizo sifiwa zipo chini ya TARURA siyo TANROADS.

Nilisikitishwa pia kuondoka kwa Prof. Mbarawa wizara ya ujenzi.

Nafikiri kinachokusumbua ni uzanzibari au/na umagufulification au wewe ni wachukia umagufulification.
 
Mimi ni kati ya watu niliosikitika kuondoka kwa Prof. Muhongo wizara ya Nishati.

Nilimpondea sana Kalemani mwanzo wa uongozi wake wizara ya Nishati na kumsifia mtangulizi wake.

Na hapo kama unefuatilia mjadala hajasifiwa raisi pekee bali muunganiko wa raisi, waziri wa uhenzi na mkurugenzi wa TANROADS ingawa baadhi ya hizo barabara zilizo sifiwa zipo chini ya TARURA siyo TANROADS.

Nikiaikitishwa pia kuondoka kwa Prof. Mbarawa wizara ya ujenzi.

Nafikiri kinachokusumbua ni uzanzibari au/na umagufulification au wewe ni wachukia umagufulification.
Kwanza hizo barabara nilizozitaja zote zipo chini ya Tanroads pia wakati ujenzi wa barabara ya Jet corner - Davis corner(Naijua vizuri kuliko zile nyingine) imeanza kujengwa 2008/2009 wakati huo Kijazi na Mfugale hawakuwepo kwenye hizo nafasi sasa huo utatu mnao uzungumzia umetokea wapi? Mimi binafsi nakubali kweli hao watu wamefanya mengi mazuri lakini msiwape sifa za watu wengine basi.
 
Nimepita kwa daladala kutoka Temeke - Lumo jet - Kinyerezi hadi Mbezi mwisho stendi ya mkoa lami tupu sijagusa vumbi.

Nikatoka Mbezi mwisho hadi Bunju kupitia Madale ni full mkeka no vumbi.

Kwa hakika Magufuli - Kijazi - Mfugale tutawakumbuka daima.

Raha ya milele uwape ee Bwana, Wastarehe kwa amani, amen!
Hawafai wote wale, walikuwa wanazua miradi mingi mingi haraka haraka ile wapige mkwanja mrefu haraka haraka; sasa Mungu fundi akwaua wote kwa haraka haraka pia!
 
Nife nikiwa nimewatendea mazuri watu hilo ndo jambo jema. Sasa jpm kila kona ya nchi ilikuwa vilio. Mazao aliua karibu yote mbaazi, korosho, tumbaku nk kisa ubabe wake. Biashara aliua kabisa na akabaki anatwambia matakwimu ya uongo eti uchumi unakua, utakuaje kiala kila kinakifu!!

Ndo mana siku ya kifo chake watu walichinja mbuzi nk. Vikana ndo usiseme ajira zote zimepigwa pini sasa hivi samia ndo anajaribu kifufua

Anatwambia, kiala kila kinakifu, vikana.

Dah mkuu ni typing error au Hasira?
 
Unachosahau Magu alikuwa Waziri wa ujenzi,Kijazi alikuwa katibu na Mfugale alikuwa mkurugenzi wa TANROADS
Kwanini wote wanekufa ndani ya miezi 5 mwaka huu?

Kabla hawajakufa kwa nafasi zao walihakikisha wanayapa madaraja na mastendi majina yao. Mfugale flyover, Magufuli bus stand na Kijazi interchange??

Kuna kitu kuhusu utatu wa uovu (evil triangle) wa hawa tutakuja kuujua siku ikifika.
 
Nimepita kwa daladala kutoka Temeke - Lumo jet - Kinyerezi hadi Mbezi mwisho stendi ya mkoa lami tupu sijagusa vumbi.

Nikatoka Mbezi mwisho hadi Bunju kupitia Madale ni full mkeka no vumbi.

Kwa hakika Magufuli - Kijazi - Mfugale tutawakumbuka daima.

Raha ya milele uwape ee Bwana, Wastarehe kwa amani, amen!
Kwani kabla yao barabara hazikujengwa? Baada ya kufa barabara zimesimama kujengwa?
 
Back
Top Bottom