Utatu wa Dkt. Magufuli, Eng. Kijazi na Eng. Mfugale katika ujenzi wa barabara nchi nzima tutaukumbuka milele

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,932
141,898
Nimepita kwa daladala kutoka Temeke - Lumo jet - Kinyerezi hadi Mbezi mwisho stendi ya mkoa lami tupu sijagusa vumbi.

Nikatoka Mbezi mwisho hadi Bunju kupitia Madale ni full mkeka no vumbi.

Kwa hakika Magufuli - Kijazi - Mfugale tutawakumbuka daima.

Raha ya milele uwape ee Bwana, Wastarehe kwa amani, amen!
 
Hii chemistry ya JPM, Kijazi na Mfugale naweza kuifananisha na ile ya Messi, Xavi na Iniesta

Ama kwa hakika kama Taifa tumepoteza wachapakazi waliojitoa kwelikweli ktk kuijenga Nchi

Tutawakumbuka daima asilani

Mwenyezi Mungu awalaze mahali pema peponi
 

84754801-2F71-4572-AA18-156D9802B676.jpeg
 
Nimepita kwa daladala kutoka Temeke - Lumo jet - Kinyerezi hadi Mbezi mwisho stendi ya mkoa lami tupu sijagusa vumbi...
Urais siyo kujenga barabara tu mkuu. Rais ni zaidi ya barabara labda unataka kutwambia kuwa jpm hakufaa kuwa rais bari waziri wa miundombinu tu.

Huwezi kuuwa, kupoteza watu na kukandamiza kila anauekupinga halafu eti barabara ndo zikuokoe. Bora limekufa tu sasa hivi tuanapumua na biashara zimerudi pia ajira sasa hivi ni choice la sivyo tulikuwa tunakufa kimyakimya
 
Barabara ya Jet corner hadi Davis corner na ile ya kutoka Mbezi hadi Goba zote zilijengwa wakati wa Kikwete tafuteni barabara nyingine alizojenga sio kumpa sifa za mwingine.
Kweli kabisa, hizo barabara zilijengwa na Kikwete. Mzee Kikwete watu wamemu-underate sana. Kafanya mambo makubwa sana yule mzee nadhani ndio kiongozi bora kiutawala baada ya Mwalimu

Tuangalie sekta moja ya afya ambapo Muhimbili ilijengwa na mkoloni almost 50% ya majengo yaliyopo pale. Alikuja Mwalimu akaongeza baadhi machache, Ruksa hakufanya chochote, Mkapa alikarabati miundombinu iliyopo ila akuongeza.

JK alijenga JKCI, New OPD, MOI na Mloganzila

Kwenye barabara za mikoa JK ndiye aliyeunganisha nchi yote kwa barabara. Amejenga airport mpya, mradi wa mwendokasi, mradi wa ubungo flyover (alianza yeye) na mingine mipya. Through JK nchi iliingia uchumi wa kati wa chini.

Nitamkumbuka na kumuenzi daima JK na katika utawala wake ndipo hata maeneo mengi ya jiji yaliendelea baada ya watu kuwa njema kiuchumi kama Madale, Malamba Mawili, Goba, Bunju, Kigamboni, Mabwepande, Kongowe ya Dar, Chamanzi n.k
 
Barabara ya Jet corner hadi Davis corner na ile ya kutoka Mbezi hadi Goba zote zilijengwa wakati wa Kikwete tafuteni barabara nyingine alizojenga sio kumpa sifa za mwingine.
Utatu unaozungumzwa hapa ni: Waziri - Katibu mkuu - DG Tanroads

Utatu huu umeanza kujenga barabara awamu ya mzee wa Lupaso, Ben Mkapa!
 
Back
Top Bottom