#UPDATES Mama mzazi wa mtoto Yusra Hassan mkazi wa Nyengedi Mkoani Lindi aliyefariki kwa kujinyonga ameeleza kuhusu kifo cha mtoto huyo huku akihusianisha tukio la kifo cha mtoto wake na imani za kishirikina
Fatuma Salum Mama wa marehemu anasema, kifo cha mwanaye hakikuwa cha kawaida kwani anamfahamu kwa namna alivyomlea na si rahisi kwake kuchukua maamuzi hayo
"Sielewi nnapoambiwa mwanangu amejinyonga hakuwa na hasira na hata alipokosea nilikuwa ninamuadhibu lakini hakuwahi kufanya kitu kama hiki" Fatuma Salum, Mama mzazi wa Yusra
Binti huyo mwenye umri wa miaka 11 inaelezwa kuwa tarehe 17 mwezi wa 5 alishindwa kwenda shule kwa kigezo kuwa anaumwa, ambapo alifanya kazi za nyumbani na kufua nguo zake ambapo muda wa saa 5 alijinyonga kwa kutumia nguo na kufariki .
Je,nini kweli mtoto wa miaka 11 anaweza kujinyonga au kuna nyuma ya pazia.