Utata wa tafsiri wa sheria ya uchaguzi?

mmaroroi

JF-Expert Member
May 8, 2008
2,960
544
Sheria ya uchaguzi inaruhusu mpiga kura kusimama mita 100 baada ya kupiga kura.Lakini Tume ya Uchaguzi inasisitiza mpiga kura akisha piga kura aondoke kituoni.Hii maana yake nini?
 
Janja ya Mwema kupalilia kitumbua chake.

Mwema aangalie sana shemeji yake(JK) asimuaribie CV yake kwani Watanzania hawadanganyiki tena baada ya miaka 50 ya kudanganywa na uongozi wa CCM.
 
Sheria ya uchaguzi inaruhusu mpiga kura kusimama mita 100 baada ya kupiga kura.Lakini Tume ya Uchaguzi inasisitiza mpiga kura akisha piga kura aondoke kituoni.Hii maana yake nini?

NEC tayari wamekwisha kutoa ufafanuzi ya kuwa ni haki ya wapigakura kuwepo kwenye vituo mita 100 ili kujionea mwenendo mzima wa zoezi la kupiga kura..............IGP hawezi kujitungia sheria zake azitakazo mwenyewe............................
 
Janja ya Mwema kupalilia kitumbua chake.

Namwonea huruma sana Mwema. Anaonekana ni mtu mzuri na ana mipango mizuri ya kuboresha jeshi la polisi tofauti na mtangulizi wake Mahita. Lkn shemeji yake aliyempa nafasi hiyo, hana hata chembe ya miiko ya uongozi, anaingiza familia katika uongozi. Mimi naamini ikulu kama ofisi kuu ya nchi, ndio sehemu ya kwanza kuweka miiko na maadili ya kazi. Kama kila mtu akienda na mke/mme na watoto wake ofisini kwake. ofisi zitakuwa vipi? Matokeo yake pamoja na umahili wa kazi wa Mwema, watu tutmchanganya kwenye kundi la mama Salma (mke), Ridhiwani(Mtoto), Makamba ( rafiki) na hatimaya Mwema (Shemeji) wa Rais.
 
Back
Top Bottom