Yah, you're right lakini niliwalenga zaidi wapiganaji kuliko Kabila kutokana na ukweli kwamba, kila tour ambayo Che Guevara alikuwa anaifanya; kuanzia ile ya kwanza kabisa wakati akiwa mwanafunzi ya kutoka kwao Argentina hadi Miami na ile tour yake ya mwisho kwenda Bolivia; zote hizi alikuwa anaziandikia memoirs/biography. Na kwenye memoir yake kuhusu Congo, hakutafuna maneno, alisema wazi kwamba walishindwa kwa sababu ya incompetence of rebel fighters.Nadhani tunaongea lugha moja. Mfano lazima uanzie kwa kiongozi. Kama yeye ni mla bata, bila shaka wapiganaji watakuwa hivyo hivyo. Kwa nini wafe wakati wanajua kiongozi wao ni mpenda starehe? Angekuwa nao bega kwa bega, wangepata morali ya mapigano na kuwa tayari kujitolea.
Nadharia hii ni sawa na vita ya rushwa hapa kwetu Tanzania. Tusidanganyane hata siku moja. Wadogo hawali rushwa kama wakubwa hawafanyi hivyo. Na kama wadogo wakijaribu kufanya hivyo, kazi ya kuwadhibiti ni rahisi kama wakubwa wapo safi.