Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 16,997
- 20,329
Eduardo Mondlane (Mwanzilishi wa chama cha kupigania Uhuru Msumbiji cha FRELIMO) akiwa na Ernesto Che Guevara katika ofisi za FRELIMO jijini Dar es salaam mwaka 1966.
Che Guevara alikuwepo Dar es salaam kwa miezi 5 kati ya mwaka 1965 hadi 1966. Akiwa Dar Che Guevara alitumia jina la Siri (code name) "TATU" kukwepa majasusi wa nchi za Kimagharibi. TATU ni jumla ya herufi katika jina C, H na E (CHE).
Ilikuwa ni katika nyakati za kiwango bora kabisa cha Ujasisi Tanzania chini ya Mzena, CIA, M16 na BOSS walikuwa wakitumia kila mbinu kuivuruga Tanzania lakini walikwama.
Alikuwa mteja wa mara nyingi katika mgahawa wa Zahir uliopo Kariakoo mtaa wa Msikiti jijini Dar es salaam (mgahawa huu bado upo) na aliishi katika Ubalozi wa Cuba. Kutoka Dar, Che alielekea Congo.
Eduardo Mondlane aliuwawa kwa bomu jijini Dar es salaam ambalo lilitegwa katika kitabu alichotumiwa toka Ujerumani Magharibi na alizikwa makaburi ya Kinondoni. Nafasi yake ya uongozi wa FRELIMO ilichukuliwa na Samora Machel ambaye alikuwa muhudumu wa tiba ya vidonda jeshini.
Kifo chake bado kina utata, dhana nyingi zikijengwa, lakini ilikuwa ni lazima afe ili Machel awe rais kwani zilikuwa ni dakika za mwisho kuelekea Uhuru wa Msunbiji.