Analogia Malenga
Platinum Member
- Feb 24, 2012
- 5,292
- 10,842
Hii nchi tutarudi kwenye mambo ya kurogana.Kumeibuka utata kufuatia taarifa za mwanamke mmoja, mama wa watoto wa wawili, kudaiwa kujinyonga katika mahabusu ya polisi jiji jijini Dar es Saalm, huku ndugu wa marehemu wakitilia shaka taarifa hiyo ya polisi.
Wakati Jeshi la Polisi likidai Stella Moses (30) amejinyonga akiwa kituo cha polisi Mburahati jijini Dar es Saalm, nduguze wametaka ufanyike uchunguzi na hawatachukua mwili hadi ukweli ufahamike.
Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni, Ramadhan Kingai aliliambia gazeti hili kuwa mwanamke huyo alijinyonga na polisi wa kituo cha Mburahati waliupeleka mwili huo na kwenda kuuhifadhi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Kwa mujibu wa Kingai tukio hilo lilitokea Jumatatu Desemba 21 lakini ndugu wa mwanamke huyo wameliambia gazeti hili kwamba Stella alifariki Jumapili Desemba 20 jioni, siku ambayo alijisalimisha kituoni hapo baada ya kupata taarifa kwamba anatafutwa.
Walisema walipompelekea mtuhumiwa huyo chai Jumatatu saa 2 asubuhi, waliambiwa na polisi kuwa wamechelewa na hivyo wakatakiwa kurudi saa tano.
Walipokwenda tena muda walioahidiwa waliambiwa waende ndugu yao akijaribu kujinyonga na amepelekwa Muhimbili, hivyo wamfuate huko.
Kwa mujibu wa msemaji wa familia, walipofika Muhimbili walielezwa kuwa ndugu yao alifikishwa akiwa amwikwishafariki dunia na mwili wake ulipelekwa na polisi saa 5:27 usiku.
Kutokana na utata wa mazingira ya kifo hicho, ndugu hao wamewenda kuonana na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa kupeleka malalamiko yao kufikisha malalamiko na kudai uchunguzi wa kifo hicho.
Mambosasa alilieleza gazeti hili kuwa baada ya kupokea malalamiko hayo, atafungua jalada la uchunguzi kubaini ukweli juu ya tukio hilo.
“Mimi kazi yangu ni kuchunguza, nimepokea malalamiko yao leo (jana) na hatua inayofuata ni kufungua jalada kwa ajili ya kuchunguza,” alisema Mambosasa.
Kwa upande wake Kingai alisema Stella alijinyonga kwa kutumia nguo aliyokuwa amevaa,” inaonekana alikuwa na madeni mengi ndiyo maana amejinyonga. Tumechunguza tukio hilo haikuwa uzembe wa askari wetu kwani wakati anaingia mahabusu taratibu zote zilifanyika ikiwemo kupekuliwa.”
Soma zaidi gazeti la Mwananchi Desemba 23, 2020
mahabusu alikuwa peke yake?Kwa taratibu za mahabusu na hali iliyopo kwenye vyumba vyao ni ngumu sana kujinyonga.
Chu&*pp<iamejinyonga kwa kutumia nguo!
eeh Mungu nisaidie na mm nimalize haya madeni maana ni km mzigo unaonielemea.. ila kujinyonga kisa madeni HAPANAAAA. wabongo tuna roho ngumu sana za ustahimilivuu wa madeni hata yaweje.Kumeibuka utata kufuatia taarifa za mwanamke mmoja, mama wa watoto wa wawili, kudaiwa kujinyonga katika mahabusu ya polisi jiji jijini Dar es Saalm, huku ndugu wa marehemu wakitilia shaka taarifa hiyo ya polisi.
Wakati Jeshi la Polisi likidai Stella Moses (30) amejinyonga akiwa kituo cha polisi Mburahati jijini Dar es Saalm, nduguze wametaka ufanyike uchunguzi na hawatachukua mwili hadi ukweli ufahamike.
Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni, Ramadhan Kingai aliliambia gazeti hili kuwa mwanamke huyo alijinyonga na polisi wa kituo cha Mburahati waliupeleka mwili huo na kwenda kuuhifadhi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Kwa mujibu wa Kingai tukio hilo lilitokea Jumatatu Desemba 21 lakini ndugu wa mwanamke huyo wameliambia gazeti hili kwamba Stella alifariki Jumapili Desemba 20 jioni, siku ambayo alijisalimisha kituoni hapo baada ya kupata taarifa kwamba anatafutwa.
Walisema walipompelekea mtuhumiwa huyo chai Jumatatu saa 2 asubuhi, waliambiwa na polisi kuwa wamechelewa na hivyo wakatakiwa kurudi saa tano.
Walipokwenda tena muda walioahidiwa waliambiwa waende ndugu yao akijaribu kujinyonga na amepelekwa Muhimbili, hivyo wamfuate huko.
Kwa mujibu wa msemaji wa familia, walipofika Muhimbili walielezwa kuwa ndugu yao alifikishwa akiwa amwikwishafariki dunia na mwili wake ulipelekwa na polisi saa 5:27 usiku.
Kutokana na utata wa mazingira ya kifo hicho, ndugu hao wamewenda kuonana na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa kupeleka malalamiko yao kufikisha malalamiko na kudai uchunguzi wa kifo hicho.
Mambosasa alilieleza gazeti hili kuwa baada ya kupokea malalamiko hayo, atafungua jalada la uchunguzi kubaini ukweli juu ya tukio hilo.
“Mimi kazi yangu ni kuchunguza, nimepokea malalamiko yao leo (jana) na hatua inayofuata ni kufungua jalada kwa ajili ya kuchunguza,” alisema Mambosasa.
Kwa upande wake Kingai alisema Stella alijinyonga kwa kutumia nguo aliyokuwa amevaa,” inaonekana alikuwa na madeni mengi ndiyo maana amejinyonga. Tumechunguza tukio hilo haikuwa uzembe wa askari wetu kwani wakati anaingia mahabusu taratibu zote zilifanyika ikiwemo kupekuliwa.”
Soma zaidi gazeti la Mwananchi Desemba 23, 2020
kwa hii serikali yetu! na hili litapita.Tulipokua kwenye uchumi wa chini tulikua na amani, huu uchumi wa kati umeondoa furaha na matumaini yetu kabisa.
Rafiki zetu China pia hawathamini haki za binadamu. Ukiwa chini ya vyombo vya ulinzi iwe mahabusu au magereza unaweza kuwa marehemu dakika yeyote.kwa hii serikali yetu! na hili litapita.
Your comment looks like sitire and sarcasm. Look back at your DPKAMA WAMEIBA UCHAGUZI NA TUPO KIMYA, KUNYANG'ANYA HAKI NA UHURU WETU NI JAMBO DOGO ZAIDI KWAO.
Dah...ni ujinga tu kujiua kwa sababu ya madeni….wakati mtu unaweza kuishi kwa figo moja bila tatizo lolote...Kule Iran ambako figo zinauzwa kihalali….figo moja bei yake ni kati ya shilingi milioni 120 hadi 300 kutokana na ubora ...halafu wewe unajiua...unafukiwa na figo zako 🤣 🤣🤭eeh Mungu nisaidie na mm nimalize haya madeni maana ni km mzigo unaonielemea.. ila kujinyonga kisa madeni HAPANAAAA. wabongo tuna roho ngumu sana za ustahimilivuu wa madeni hata yaweje.
china ni roll model wa mkuluRafiki zetu China pia hawathamini haki za binadamu. Ukiwa chini ya vyombo vya ulinzi iwe mahabusu au magereza unaweza kuwa marehemu dakika yeyote.
Hata me nlitaka kuuliz hvyohvyomahabusu alikuwa peke yake?