Utata mtupu magari ya mawaziri: Nani alinunua?

Msharika

JF-Expert Member
May 15, 2009
939
225
Sadick Mtulya

WAKATI mawaziri na manaibu wawaziri wakikabidhiwa magari mapya, baada ya kuapishwa Jumamosi iliyopita, serikali imeibuka na kusema sio mapya ni ya zamani.

Kauli hiyo inaibua utata kutokana na kuwa baada ya kuapishwa viwanja vya Ikulu na Rais Jakaya Kikwete, kila waziri alikabidhiwa dereva mpya na gari jipya aina ya Toyota GX V8, badala ya gari aina ya Toyota VX V8 iliyokuwa ikitumiwa na mawaziri waliopita.

Ununuzi wa Toyota GX V8 mpya, unashiria serikali bado haijawa tayari kuunga mkono msimamo wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambaye amekuwa akisikika akitaka kusitishwa ununuzi wa magari ya kifahari ili kupunguza matumizi ndani ya serikali.

Toyota GX V8 moja huuzwa kati ya Sh210 milioni hadi Sh240 milioni, hukuToyota VX V8 moja inauzwa sio chini ya Sh180 milioni.

Akizungumza na Mwananchi jana, Katibu Mkuu wa iliyokuwa Wizara ya Miundombinu, Omari Chambo, alisema magari hayo sio mapya na kwamba, yaliyotumiwa na mawaziri waliopita.

Rais Jakaya Kikwete ameigawanya iliyokuwa Wizara ya Miundombinu na kuwa wizara mbili; Wizara ya Ujenzi na Wizara ya Uchukuzi.

“Yale magari sio mapya, yalikuwepo. Kwanza uliyaona au unasema tu, hamjayachunguza vizuri jamani, fanyeni uchunguzi,’’ alisema Chambo na kukata simu.

Mawaziri wote na baadhi ya manaibu walikabidhiwa magari hayo (GX V8), huku manaibu wengine wakikabidhiwa VX V8.

Sababu ya baadhi ya manaibu mawaziri kukabidhiwa VX V8 badala ya GX V8, ni kutokana na kutokamilishwa kwa taratibu za kutokamilika.

Mmoja wa manaibu mawaziri (jina tunalo), alikabidhiwa VX V8 iliyokuwa ikitumiwa na aliyekuwa Waziri wa Maendeleo ya Mifungo na Uvuvi, John Magufuli, ambaye sasa ni Waziri wa Ujenzi.

Gazeti moja la kila siku (si Mwananchi) limeeleza kuwa ununuzi wa magari hayo, umegharimu serikali Sh9.3 bilioni na kwamba, takwimu za iliyokuwa Wizara ya Miundombinu zinaonyesha kuwa hadi kufikia mwishoni mwa mwaka wa fedha wa 2005/06 magari makubwa ya kifahari yapatayo 6,000 yalikuwa yamenunuliwa na serikali kwa gharama inayokadiriwa kufikia Sh160 bilioni.

Miongoni mwa magari hayo ni Toyota Land Cruiser (VX/ GX V8, Prado) yapatayo 1,655, Nissan Patrol na Land Cruiser 885, Mitsubishi Pajero 400 na mengineyo.

Tangu kipindi cha serikali ya awamu ya tatu chini ya Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, kumekuwepo na mjadala kuhusu matumizi makubwa ya serikali hasa katika ununuzi wa magari ya kifahari kutokana na kuendeshwa kwa gharama kubwa.

Wadau wengi wanataka viongozi watumie magari ya kawaida kama ilivyo kwa nchi ya Kenya na Rwanda
 

samora10

JF-Expert Member
Jul 21, 2010
7,587
2,000
Hivi wakipewa grand vitara/escudo au hata corrola hawawezikufanya kazi? kwani hizo V8 wanazitumia kufanyia nini zaidi ya kuwapeleka kazini asubuhi na jioni na airport kama wana safari?:whoo:
 

Byendangwero

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
871
0
Uundwaji wa baraza kubwa la mawaziri pamoja na hili la ununuzi wa magari mapya tena yenye bei mbaya ni viashiria tosha ya kwamba serikali ya sasa kama ilivyokuwa ile iliyotangulia vipaumbele vyake vimejikita katika kujihudumia wao kwa wao, matatizo yanayowakabili wananchi wa kawaida hawana habari nayo.
 

Pakawa

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
6,797
2,000
Huu upuuzi wa hii nchi mbona nchi zilizoendelea hawana ujinga huu wa kupeana magari kama peremende. Hivi ni lini hii mijitu itaelewa?? Unampa waziri gari kwa gharama ya serikali why??? Magari wangeweza kupewa lakini wangekuwa wanayafinance na interest juu tuone kama watayataka hayo magari.

Halafu anapewa na dereva wa kumwendesha mpaka kumpeleka kwa vidosho wake halafu akiandikwa kwenye gazeti anaanza kelele. Hii nchi kama viongozi wake wamekunywa ACID. Tusker Baridiiii unalilia ****** mimi nalilia chini ya uvungu wa kitanda maana ni aibu hata kumweleza mtu mwenye akili zake halafu kutwa nzima na bakuli kuomba omba kama wendawazimu fulani hivi.

Nina hasira na hawa watu. Haya mlioichagua CCM makali ndio haya yanaanza mpaka 2015 mtakuwa wote mmechakaa kupita maelezo.
 

Jasusi

JF-Expert Member
May 5, 2006
11,522
2,000
Siyo magari tu. Mawaziri wanalipiwa pia petroli wanayotumia kwa matanuzi yao. Halafu kinachonishangaza hizo Toyota sijui GX au VX mbona bei zake huku Marekani hazizidi $75,000? Lazima kuna mshiko hapo.
 

MAMA B

Member
Nov 1, 2010
29
0
we jasusi kweli uko marekani.........ivi hujui kama kuwanunulia magari mawaziri ni tenda ya hao hao wakubwa katika kupeana 10%......watakwambia hii ni model sijui ya mbinguni na ndio maana bei iko juu.......itasaidia kwenda vijijini wakati wanaenda wakati wa uchaguzi........!lazma muweke cha juu ili mgawo uwapitie wahusika wote waliomwaga hela zao nyingi wakati wa uchaguzi na hii ndio bongooooooooo!
naomba usirudi bongo maana ukirudi utapata kichefuchefu kila sehemu...sio ununuzi tu.....
THE SYSTEM IS NAKED....
 

Kabembe

JF-Expert Member
Feb 11, 2009
2,551
2,000
Huyo Pinda hana lolote,kazi kulalamika tuuu kama mwananchi wa kawaida,Magufuri waziri wa kawaida lakini alijaribu na kufanikiwa kuwabana wakubwa wenzie kwa kubadilisha magari yote ya umma kuwa SU,STJ,STk n.k badala ya namba binafsi but Pinda have never tried anything!!! Yaani ni goigoi ayefaidika na mfumo mbovu wa utawala,anajifanya mtoto wa mkulima ili Wadanganyika wamwone kama mwenzao huku yeye akiendelea kuitafuna nchi nj wezi wenzie
 

paty

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
1,340
2,000
mungu okoa taifa lako...

jamani just imagine bibi kizee mjane analea watoto/wajukuu yatima , mlo wa wasiwasi.... ila kila anachonunua anakatwa VAT..ili hawa jamaa wafanye anasa zao....
FORGIVE US OOOH LORD
 

Amoeba

JF-Expert Member
Aug 20, 2009
3,296
0
Naombeni BAN kabla sijaandika hisia zangu kwa uwazi!
-Hawa jamaa hawaongozi watu, wanaongoza mabata!
-65% ya wabongo ni watu wenye akili finyu, hivyo mabadiliko litakuwa suala gumu.
-Huo ni usen**

Siku ile mama yake pinda alikuwa ananyenyekea na kubembeleza "utuletee zana bora, tunalima kwa mkono sasa tumezeeka", huyu mama anawakilisha majority ya watanzania wa shambani! Ufahari unaua nchi, kwani mkiendeshwa kwenye cruser ya M70 tatizo? Pinda angekuwa mpiganaji halisi angelikataa GX akaonesha mfano, gari anayotumia ina thamani kuzidi nyumba 10000 za kijijini kwao! These bstds!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom