mjerumaniwapahi
JF-Expert Member
- Sep 4, 2014
- 378
- 270
Habari za jumapili wanajf wenzangu
Mimi ni kijana wa miaka 30, nilipata utata pale nilipomaliza elimu kwani bibi yangu mzaa mama aliniita kijijini
Nilipofika tu bibi aliniambia mjukuu wangu pole kwa mihangaiko yako ya miaka nenda rudi
Mihangaiko yangu ni mingi sana nilifiwa na mzazi wa kiume (baba) nikiwa na miaka 6 na nikafiwa na mama mzazi nilipofika darasa la 7 nikiwa na miaka 15 pia nikiwa mtoto wa pekee katika familia yangu hiyo na baada ya kifo cha wazazi nilisoma kwa mipango ya mungu mpaka nikamaliza masomo
Utata ulikuja pale bibi yangu mzaa mama aliponiambia mjukuu wangu nina siri ya maisha yako ..nikamuomba aniambie hiyo siri akadai niwemvumilivu na atakayo yasema
Bibi aliniambia baba yako aliyefariki siyo baba yako mzazi kwani mama yako aliolewa akiwa mjamzito na baba yako mzazi yupo hai na nitakusaidia kuonana nae ila ibaki siri yenu ndipo nikakubali na juhudi za kuonana zikafanyika na tukaonana na kiukweli mm na huyo mzee tunafana kila kitu kuanzia kimo ,sura, rangi mpaka sauti na tuliongea mengi japo mimi sikuhitaji chochote toka kwake ila tulikubaliana iwe siri tu maana tayar mimi nina ndugu zangu wa marehem baba mwinngine
Na tutabaki kama marafiki tu na huyu baba wa sasa ila tatzo siri hii haiwezi kudumu maana mama angu mdogo anaijua ,bibi na mimi tena... Nijuavyo mm siri ni ya mtu mmoja
Pia marehemu mama angu aliwahi kuniambia nikiwa mdogo kuwa mwanangu nitakuja kukwambia jambo lililojificha katika maisha yako ila alifariki kabla hajaniambia
Hivyo basi ndugu zanguni wanajf mwenzenu huwa naishi kwa utata mno endapo siri hii itajulikana kwa ndugu wa upande wa baba nini kitatokea hali yakuwa wahusika wakubwa walushatangulia mbele ya haki
Pia upande wa baba wa ukubwani wapo ambao walishadokezwa na siri hii na baba yao
Kama una ushari, maoni unaweza kuutoa
Nawatakieni jumapili njema