Utata juu ya mapato ya CCM Tanzania

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
11,185
Reaction score
24,565
Hiki chama kinapata wapi mapato yake hususani hawasemi? Wanaweza kusema labda ni wanachama mimi nasema la hiki chama kinapata wapi mabilioni ya kuwapa wasanii kama kina Diamond na wengineo wengi.

Bora hata vyama vya upinzani CHADEMA for instance mbali na ruzuku wanapata pia misaada kutoka vyama rafiki nje lakini mbali na CCM nadhani si ruzuku tu.

Huenda pesa zinachotwa serikalini hakiwezekani chama hakijulikani mapato yake yanatoka wapi ambapo wanagharamia mabilioni ya pesa kwenye vijimikutano yao.

Isiwe ikawa ni kodi zetu
 
SERIKALINI?????
 
Wana miradi mingi
 
Vipi MKUU UNAFAHAMU JUU YA MATUMIZI YA RUZUKU NA HIYO MISAADA KWA CHADEMA?????maana hakuna cha maana kwenye hiki CHAMA kinachoonekana mpaka sasa ZAIDI YA KUONA WATU WACHACHE WATUNA MATUMBO TU .....ebu tuanzie hapo kidogo Afu na mimi ntakusaidia juu ya Vyanzo vya mapato ya CCM na matumizi yake...........
 

Mkuu naona kana unauliza vumbi darini. Huko hazina wananyofoa kwa lugha watarudisha. Wakikosa inaandikwa kwenye bad debtors.
 
Mkuu Max anateswa kwa sababu kawakatalia CCM kununua JF kwa billioni 10. Jiulize wanazipata wapi?
 
Mkuu vyanzo vya mapato vya ccm vyote ni Mali za umma ukawa ukiingia madarakani vyote vinarudi serekalini
 
Kosa, umeshindwa mtihani
 
Yeye kauliza mapato ya CCM ukitaka ya Chadema anzisha uzi wake utajibiwa.
 
Di dili zote kubwa za kifisadi ccm hupata mgao, ndio maana mafisadi papa hawawezi kufikishwa mahakamani
 
Ccm ndio chama tajiri barani Africa hebu jaribu kufuatilia tu kwa mkoa unaoshi wewe Mali za ccm tu then rudi tena kuandika hapa
 
Ccm ndio chama tajiri barani Africa hebu jaribu kufuatilia tu kwa mkoa unaoshi wewe Mali za ccm tu then rudi tena kuandika hapa
hahaha we jinga kwel mali zipi za kuwapa mabilioni? jee ni yale majumba mabovu Ya maofisi mlojenga kule?
hivyo viwanja mmeweka vitega uchumi gan?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…