Utaratibu wa kutolewa vyeti upoje?

Utaratibu wa kutolewa vyeti upoje?

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2022
Posts
33,977
Reaction score
67,611
Habari,

Mimi napenda kujua utaratibu sikuizi wa utoaji vyeti upoje?

Zamani mtu upo kigoma umesoma dar unatuma barua ya maombi ya kutumiwa cheti chako kwa njia ya posta unakipata sikuizi shida nini?

Mbona kama tunakomoana maana unalazimika kukopa hela umpe mwanafunzi aende kufwata cheti chake hukoo manyoni shida nini?

Naomba kujua hilo mdogo wangu kanichanganya akili kabisa hapa sijalipa ada za watoto yeye naye anatak laki ya nauli kwenda kufwata cheti chake.
 
Utaratibu wa siku hizi, unaenda shuleni wewe mwenyewe kukifuata cheti otherwise kuwe na sababu nyingine zenye mashiko zilizokufanya ushindwe kufika,nahisi hua wanafanya hivi.

1. Kutoa cheti kwa mtu hudika na yeye kuidhinisha/kusaini kua amekipata.

2. Hii ni kuku bana wewe kama ulikua na deni shuleni huezi kupewa cheti hadi deni lilipwe
 
Lengo ni usalama wa cheti, inaweza ikatokea mtoto au jamaa amekuudhi unaenda kuchukua cheti unachoma moto. Yeye akikihitaji anaambiwa ameshachukua ndugu au jamaa yake na italeta usumbufu. Afike mhusika au muwakilishi Kwa idhini ya mhusika.
 
Habari,

Mimi napenda kujua utaratibu sikuizi wa utoaji vyeti upoje?

Zamani mtu upo kigoma umesoma dar unatuma barua ya maombi ya kutumiwa cheti chako kwa njia ya posta unakipata sikuizi shida nini?

Mbona kama tunakomoana maana unalazimika kukopa hela umpe mwanafunzi aende kufwata cheti chake hukoo manyoni shida nini?

Naomba kujua hilo mdogo wangu kanichanganya akili kabisa hapa sijalipa ada za watoto yeye naye anatak laki ya nauli kwenda kufwata cheti chake.
Kijana umekuja na moto mno!! Unayetaka kufuata cheti ni wewe mwenyewe halafu unazuga eti umelipa ada za watoto. Wewe mwenyewe mbona bado mtoto tena upo kwa wazazi. Nimesoma posts zako nimebaini ni kavulana kadogo bado upo chini ya himaya ya wazazi.

Karibu sana Jamiiforums!!
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kweli na siwez toka hapa home
 
Back
Top Bottom