KERO Chuo cha SAUT-MWANZA wanasumbua kutoa vyeti kwa wahitimu, pia wanachanganya matokeo

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Tupo kwenye sintofahamu, Chuo cha SAUT-MWANZA mpaka sasa hakijatupa Vyeti wahitimu wa Mwaka 2023.

Ukienda kufuatilia wanasema tusubiri wakidai vyeti havijafika, wakati huohuo wengine wamepata, sasa tunashindwa kuelewa wanatumia utaratibu gani wa kutoa vyeti.

Baadhi ya waliopata nao pia wamekutana na changamoto ya TRANSCRIPT kuchanganywa masomo mfano kwa waliosoma BAED (Bachelor of Arts with Education) unakuta wameandikiwa Kiswahili & Literature lakini transcript unakuta imeandikwa Geography & Linguistic.

Tunapata shida Watu tunatoka mbali kufuata cheti unakutana na changamoto za ovyo, inakera sana.
 
Back
Top Bottom