Achana na miundombinu ya stand mpya na vibaka.. "kwanini mabus yalale njiani?"
Si yamefungwa vidhibiti mwendo? Kama ni utekaji polisi si kazi yao kupambana na majambazi?
Sumatra wana kambia utaratibu huo ni lazima pia wizara nyingine zihusishwe kwani enda ajari itatokea saa kumi afrajili vyombo vya uokozi vitaweza patikana? je hospital muda huo za kupokea wahanga zitakuwa wazi?japo hata hizo zinazotokea mchana tu ni majanga msaada ndio huo watu wana kandamizwa na contena vyombo vya uokozi hakuna!!Hivi kama mabasi yanaingia dar mpaka saa nne usiku, maana yake yametembea toka saa kumi na mbili jioni mpaka saa nne hiyo usiku gizani, tena madereva wakiwa wamechoka ila hamna ajali wala ujambazi. Kwa nini kama imeshindikana kusafiri muda wowote usiku basi mabasi hayo yaruhusiwe kuanza safari hata saa tisa usiku na madereva wanakuwa fresh zaidi? Mfano wa dar wakitoka saa tisa au kumi alfajiri, wakifika morogoro saa moja asubuhi si haba kwamba huko waelekeako watawahi fika.
Urasimu......Ndipo ninapoingiwa na hofu na wanausalama barabarani, pamoja na uwepo wa ving'amuzi lakini kusimamishwa ni kila walipo askari, kwanini kisitumike kituo kimoja tu katika kila mkoa
Nakubaliana na wewe kabisa maana na mimi hiyo kero ilinikuta ni zaidi ya mateso ni afadhali kupanda ndege kuliko mateso utakayokutana nayo kwenye basiSalaam wakuu,
Kwa masikitiko makubwa naomba nizungumzie huu utaratibu wa kulaza mabasi ya abiria nzega,sijajua shida ni nini wakati unatoka mikoa mingine kuja dar es salaam basi linafika siku hiyo hiyo lakini ajabu ukiwa unatoka dar kwenda mikoa hasa ya kanda ya ziwa basi linalala nzega na safar inaendelea kesho. Si vibaya kwa basi kulala stendi "MPYA" ya Nzega ila niseme tu mazingira ya hiyo stendi mpya ya Nzega sio rafiki kabisa,kwanza huduma za vyoo ni mbovu sana ,kuna matundu matatu tu ya vyoo na bafu moja kwa kila jinsia. Haitoshi vyoo ni vichafu sana yani wale wasimamizi wanajua kuchaji tu pesa ya huduma na sio kusafisha vyoo,hii ni hatari kwa afya zetu hasa sisi wanawake.
Kitu kingine ni abiria kulazimika kulala wamekaa kwenye siti za basi kwani hakuna nyumba za wageni maeneo ya karibu ,sasa hapo ukiamka kesho unakuwa kama zombie akili imezubaa kabisa,.
Cha mwisho usalama wa abiria stendi mpya ya Nzega ni mdogo mno ,kuna vibaka pale sijapata kuona ole wako utoke uende uwani unakuta washapiga sachi begi.
Ushauri wangu serikali ifanye juhudi za maksudi kuboresha stendi mpya ya Nzega,abiria tunapitia mateso makubwa.vyoo viongezwe,walau boma LA kuwasitiri "walala nje" liwepo,usalama wa wasafiri uimarishwe ili basi Watanzania waendelee kuongeza maksi katika utawala wa awamu hii ya hapa kazi tu.
Muwe na Jumapili njema
Mkuu kwani Siku hizi hawalali tena Shinyanga?Salaam wakuu,