Utaratibu mpya tcu - maoni yangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utaratibu mpya tcu - maoni yangu

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Yona F. Maro, Apr 13, 2010.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Apr 13, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Siku chache zilizopita TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA ilianzisha rasmi utaratibu mpya kwa wanafunzi wanaotaka kujiunga na vyuo vikuu kwa njia ya mtandao na simu za viganjani .
  Kwa kweli huu ni utaratibu mzuri tu na utarahisisha mengi ambayo wanafunzi wengi walikuwa wanapata tabu katika kufuatilia na kujua taarifa zao zingine kwa gharama nafuu

  .
  Pamoja na pongezi hizi kuna baadhi ya mambo inabidi tuyaangalie kwa mbali kidogo sio kwamba natoa makosa hapana haya ni mawazo yangu tu ambayo yanaweza kuijenga hii taasisi vizuri na pengine hata taasisi zingine kufuatia .


  Kwenye upande wa tovuti kwa ujumla maandishi yake hayajakaa vizuri na hayaendi kwenye mtiririko mmoja unaofaa kwa ajili ya mtumiaji wa kawaida wa tovuti mtiririko huo umechangiwa zaidi na lugha iliyotumika katika kuandika baadhi ya vitu kwenye tovuti hiyo mfano kuna maneno ya kifupia kama TZ mengine yaliyokatwa Kama News Letter na mengine mengi yanayofuatia .


  Hata suala la Viunganishi kwenye anuani za tovuti za vyuo vingine limekuwa gumu angalia http://www.tcu.go.tz/universities_colleges.html vyuo vingi hapo vina tovuti kulitakiwa kuwe na anuani zao moja kwa moja badala ya http://www.tcu.go.tz/links.html hii ilifaa kuwekwa viunganishi vya tovuti kama za wizara ya elimu , taasisi ya elimu , Necta na kadhalika .


  Kungekuwa na kiunganishi kingine cha kuunganisha vyuo vikuu vyote nchini ndani ya tovuti hiyo pamoja na bodi ya mikopo ili kumpa mtu njia rahisi zaidi za kufanya kazi zake badala ya kufungua anuani mbalimbali kama anatafuta taarifa Fulani .


  Suala la lugha limekuwa ni tatizo sugu bado kwenye sehemu zetu kadhaa watu wanaendeleza lugha za nje basi ni bora wangeweka mtu achague lugha kama ni Kiswahili au kingereza badala ya lugha moja kama kweli tunataka kuendeleza lugha hii kwenye matumizi ya teknohama basi sehemu kama hizi ni nzuri sana kwa ajili ya kuendeleza zaidi
  Kitu kinachohusu umma kama hichi ni vizuri kufanyiwa Review na wadau wengine kabla ya kupeleka kwa jamii , Kuna wadau wa teknohama kwenye idara mbalimbali za serikali na hata baadhi ya majukwa ya mitandao wapo hawa wangeshirikiwa wangeweza kuleta changamoto kubwa hichi ni kitu kinachokosekana sehemu nyingi za kazi nchini  Kuna suala la Privacy Policy kwa sababu tovuti hiyo inachukuwa taarifa za watu tena kwa kushirikiana na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom ni vizuri sana wangeandika Hiyo Policy wauambie umma sasa jinsi taarifa zao zitakavyotumika kwa ajili ya ulinzi wao binafsi na mengine mengi , suala hili linaweza kusababisha watu haswa wale wan je ya nchi kutotumia mtandao huo bila kuelezwa .


  Kwenye utaratibu wa kuomba hatua ya B itakuwa na tatizo kwa baadhi ya watu ambao hawatumii kivinjari aina ya firefox au wanaotumia internet explorer matoleo ya nyuma ilibidi kueleweka idadi kubwa ya watu wanatumia Internet Explorer Toleo la 6 zaidi kwa upande wa simu za viganja wengi ni Opera .


  Na kompyta nyingi kama ni Mgahawa wa Mtandao kwa mfano zimefungwa kufanya baadhi ya vitu kama hivyo kushusha vitu toka kwenye mtandao au kuoweka program hizo kwenye kompyuta kama hazipo kwa ajili ya usalama .


  Nilipoona hiyo hatua B nilikumbuka mradi wa Tuwasiliane ambao ulikuwa chini ya COSTECH angalia hapa http://www.costech.or.tz/kkk na http://stats.tix.or.tz/kkk/ naamini mradi huu ungeendelea vyema ungeweza kusaidia sana katika suala hili kwa wanafunzi
  Mambo mengine ni pamoja na kutoa elimu zaidi kwa watumiaji wa Huduma hii mpya kwa watu mbalimbali sio kwenye magazeti tu hata kwenye vyombo vingine ya habari kama radio na TV bila kusahau kwa njia ya mtandao kuna Majukwaa mengi ambayo wanaweza kusaidia kuweka Tangazo hili kwa ajili ya kufikia watu wengi zaidi tutumie nafasi hizo chache za mawasiliano tuone .


  Mwisho napongeza hatua hii iliyofikiwa na Taasisi ya vyuo vikuu Tanzania pamoja na vitu nilivyotaja hapo juu
   
 2. moto ya mbongo

  moto ya mbongo JF-Expert Member

  #2
  Apr 22, 2010
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 336
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 45
  Maoni yako ni mazuri privacy za watu lazima zilindwe twna jambo lenyewe la elimu linahitaji umakini wa hali ya juu
   
Loading...