Utapeli wa wastaafu je mashirika ya hifadhi za jamii yanahusika?

Masasaa

JF-Expert Member
Oct 23, 2015
585
623
Kumekuwa na hii shida siku za hivi karibuni kwa wastaafu, hasa ambao tayari wameshalipwa mafao yao, wanaofuatilia mapunjo hasa kwa mkoa wa Morogoro.

Hawa matapeli wanakuwa na details zote za mstaafu kuanzia mshahara wake wa mwisho, check namba yake, namba yake ya simu, kiasi cha mafao aliyolipwa na wanampigia simu kumtaka awalipe kiasi fulani cha pesa ili mafao yake yashughulikiwe na wastaafu wengi kwa kuwa wanakuwa wanazihitaji hizo peda wanaingia king.

Jumamosi iliyopita mama mkwe wangu alipigiwa simu na hao matapeli na kumwambia alipe 800,000 kwa ajili ya stamp, walipompigia walimwambia wako hazina ndogo Morogoro, kwa hiyo aende pale akawape hiyo pesa, akashituka akatupigia, tulipokuwa naye alipowapigia wakamwabia atume kwenye simu ndipo wife akachukua simu kuongea nao, huyu aliyekuwa anaongea alikuwa anaongea sauti ya kike kumbe ni dume, ambapo wife alioga matusi ya nguoni ya kutosha.

Jumatatu ya wiki hii kuna mama mmoja naye alipigiwa atoe 1.8m akenda NSSF wakasema hawana utaratibu huo, jana kuna mama kapigwa 600,000/= leo kaenda nssf wakamwambia wao hawana utaratibu wa kuomba pesa, sasa jamani hawa matapeli wanazitoa wapi hizi details za wastaafu kama sio watu wa ndani wanawapa.

Jamani NSSF, PSSF na Hazina mtatuulia wastaafu wetu kwa pressure
 
Back
Top Bottom