MIMI BABA YENU
JF-Expert Member
- Mar 1, 2019
- 295
- 679
Zaidi ya wakazi elfu 40 wa Vijiji viwili vya Dalla na Bwade vilivyopo wilayani Morogoro mkoani Morogoro wameiomba serikali kuingilia kati kurejesha ardhi yao yenye ukubwa wa ekari zaidi 1000 iliyochukuliwa kwa njia ya utapeli na aliyekuwa waziri wa Mifugo LUAGA MPINA tangu mwaka 2009.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wilayani humo wakazi hao wamesema ardhi hiyo iliyochukuliwa kwa awamu tofauti na kiongozi huyo katika kipindi cha kuanzia mwaka 2009 hadi mwaka 2017 bado haijaendelezwa huku asilimia kubwa ya wananchi wakikosa ardhi ya kilimo.
Aidha wananchi hao wamesema licha ya kupaza sauti zao ngazi mbalimbali za uongozi lakini hadi sasa bado ardhi yao imeendelea kushikiliwa na hakuna hatua zozote zilizo chukuliwa na kuomba Rais Dkt SAMIA SULUHU HASSAN kuingilia kati ili kurejeshewa ardhi yao waendeleze kilimo.
Baadhi ya Viongozi akiwemo mwenyekiti wa Kijiji cha Mbwade SALUM MALOZO amesema baada ya kiongozi huyo LUAGA MPINA kuchukua ardhi ya Kijiji Jirani sasa ameinga tena katika Kijiji chao na kuchukua zaidi ya ekari 80 nazo bila kufuata utaratibu huku kukiwa hakuna taarifa zozote zilizo mruhusu kumiliki ardhi hiyo .
Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Dalla kilichochukuliwa zaidi ya ekari 1000 MOHAMED KILIMASINDE amemfananisha kiomgozi huyo sawa na mtu mbinafsi asiye na huruma kwa wananchi wa hali ya chini.