mawelewele
JF-Expert Member
- Sep 17, 2016
- 277
- 135
Kwako Mkuu wa Mkoa wa Iringa na mamlaka husika zote zilizopo Iringa, hii taasisi bubu inayojiita iringa microfinance, wako floor ya pili ghorofa la IMMUCU, hii taasisi hakika imekuwa kero kwa walimu, kwani hutoza riba 50% kwa walimu na hivyo kutokuwa msaada kwao bali ni mateso na kutokana walimu mishahara yao midogo hujikuta wanaingia katika mtego huo, inafikia mwalimu akishindwa hufuata shuleni, kumsumbua sumbua na hata kuathiri ufundishaji wa watoto, pia hawa watu hawatoi risiti za TRA ukipeleka marejesho.
Mimi ushauri wangu, Mkuu wa Mkoa ili kuokoa elimu katika mkoa wetu wa Iringa hebu tuondolee hii taasisi inayofanya walimu wasitulie shuleni na kukimbiakimbia, kwani hawa watu hutumia hadi polisi ili kuwatisha wadaiwa wao, kwani walimu ni wanyonge na wengi wao ni waoga, pia hii taasisi haijasajiliwa, kwani inatumia TIN namba ya mtu binafsi, hawatoi risiti za TRA.