Utapeli mwingine wa Mjin City donation

mwambojoke

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
1,060
630
Wandugu naomb mjihadahri na hawa watu. Hivi ni kwanini wabongo hatujifunzi tu?? Jaribu kuingia kw website yao ,halafu pima kama kuna ukweli.

Soma muongozo vizuri kabla ya kuchangia

Mfumo ni wakuchangiana wenyewe na mzunguko wa pesa ni ndani ya siku 4. Baada ya mzunguko wa siku 4 utapokea faida ambayo ni 50% ya kiasi ulowokeza.

kiasi ambacho kitatolewa ni faida pamoja na mtaji wako. sharti la platform yetu kila mwanachama atatakiwa kua na account zaid ya moja.

kila baada ya kupokea mwanachama atatakiwa kufanya uwekezaji zaid ya 70%(imependekezwa) ya kiasi alichopokea kwa siku husika.

kuhusu usajili

kila mwanachama anapaswa kufanya usajili kabla ya kuanza kuchangia. Usajili huo unafanyika ndani ya system hii ya city donnation ambapo gharama za usajili ni 15,000/= kwa mwanachama, pesa hii italipwa mara moja tu.



Ngariba1 said

Mnataka niseme mara ngapi ndio muelewe? Kokote kwenye pesa watu huwa hawaalikani. Fursa huwa zinachangamkiwa kimnya kimnya. Ukiona unaalikwa kwenye pesa na mtu anakusihi sana uingie ili ufanikiwe, hapo hakuna pesa. Ni upatu.


Na hii ndo message yao inasambaa.


CITY DONATION

✍MUONGOZO MFUPI.

VODA NOW:
✍ M-PESA: 174328 - INVESTMENT

✍ T-PESA: 536778(filled)

TIGO NOW:
✍535174 - ATHANAS G.

kwa taarifa zaidi:
welcome
 
Back
Top Bottom