Utapeli mtandaoni: Matapeli wanajuaje namba ya Siri?

Utapeli mtandaoni: Matapeli wanajuaje namba ya Siri?

Grena

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2016
Posts
656
Reaction score
1,557
Habari zenu wakuu.

Jana mama yangu katapeliwa hela kutoka TigoPesa. Nilimsindikiza Ubungo mida ya mchana tukapanda basi kwenye ile seat aliyokaa tukamkuta mkaka amekaa dirishani kwasababu mama siti yake ni dirishani na tulikuwa tumewahi sana, akatupisha akasema nawaacha mkae pamoja kidogo mpige story siti yangu ni ya pembeni akaenda siti ya nyuma.

Baadae kidogo akarudi ikabidi niinuke nimpishe akae siti yake. Akamuuliza mama unasalio naomba nipige mama akijua ni msafiri mwenzake akampa simu, akajifanya nampigia hapokei akarudisha Simu, Mara hiyo hiyo akashuka akasema Naenda kununua vocha.

Jioni mama amefika nampigia ananambia yule mkaka hakurudi kwenye bus. Ile siti haikuwa yake alikuja kukaa mtu mwingine, nawaambia siti Ina mtu Hadi konda akaja akasema hii siti sijaikatia ticket.

Nikas-ense something is wrong nikamwambia mama ameshika simu yako na hakurudi kwenye bus kuna kitu kafanya angalia salio lako la TigoPesa. Kweli kuangalia salio limekombwa loooteeee.
Tuliangalia Taarifa ya miamala pesa imetumwa namba 0719169535 na muda uliyotumwa Ni muda ambao Tulikuwa ndani ya bus. Kweli imetuumiza sana

Usalama wa pesa zetu kwenye mitandao ya simu upoje? Hawa wezi wanajuaje namba zetu za siri?

Mimi nimeogopa kwenye simu saivi siachi zaidi ya elfu 5 na kujifanya mwema kumpa Sim mtu nisiyemjua never.

Update: Wakuu kunamdau comment 109 kaeleza vizuri kilichotokea. Ni maengineer wa mitandao wasiowaaminifu wanashirikiana na wezi Kuwapa USSD jinsi ya kutoa fedha. Ukiweka USSD option ya kuweka namba ya Siri inarukwa unatuma tu hela.

Tuweni makini kuwapa watu tusiowajua simu zetu, kujifanya msamaria mwema sometimes unaishia kulizwa.
 
Pole sana. Yawezekana mama alitoa taarifa zake za siri bila kujua.
 
Waliotoa shs ngapi? Mngepiga simu tiGO huduma kwa wateja muhifaamu hiyo namba iliyotoa pesa.
 
Hapo kama mama alifanya muamala wowote akiwa kwenye gari jamaa atakua alichungulia akaona password.

Njia nyingine huyo mwizi anamfahamu huyo mama na anajua namba yake ya siri.
 
Hakuna namna mtu anaweza kuiba salio bila kujua password
 
Hiyo ni kiini macho hata mimi sielewi kapigwaje, maana sitaki kuamini kama mama alimpa password, pia mtu mpaka aingie kwenye huduma ya tigopesa afanye muamala huoni tu
 
Aisee wezi wamechachamaa ila kuna namna mama alitoa namba za siri bila yeye kujua au laini ilikua mpya namba zake za siri "0000" ????
 
Au mama namba ya siri alisave au ilikuwa kwenye sms.
 
Hapo kama mama alifanya muamala wowote akiwa kwenye gari jamaa atakua alichungulia akaona password.

Njia nyingine huyo mwizi anamfahamu huyo mama na anajua namba yake ya siri.
Hakufanya muamala wowote. Simu ilikuwa kwenye pochi alivyomuomba akatoa akampa. Na hatumfahamu tulimkuta kwenye bus, nadhani ndo Kazi yake kujifanya abiria Halafu anatapeli kwa staili Hiyo
 
Waliotoa shs ngapi? Mngepiga simu tiGO huduma kwa wateja muhifaamu hiyo namba iliyotoa pesa.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
Tumepiga hawana msaada wowote. Wamesema hela ishatolewa hawawezi fanya chochote. Kama tunataka zaidi twende police
 
Au mchizi aliiambiwa anunue voucher kupitia Tigo PESA...baadae akajiongeza.
 
Au mchizi aliiambiwa anunue voucher kupitia Tigo PESA...baadae akajiongeza.
Amna Aliomba apige sim tu. Akajifanya anapiga Kumbe ndo anahamisha muamala.
 
Mama asijifanye kuzuga zuga. Kuna jambo la siri aliongea na huyo mpambanaji.

Mi mwenyewe niliwahi pigwa na mtu kwa sim banking laki 2 na 30, nikafanikiwa kuokoa laki 2.

30 ikaenda lakini nikamshika hawara wa mwizi wangu baada ya miezi mitatu.

Aende polisi aripoti hio namba iliopigwa kisha kitaeleweka.

Kama uko Dar nicheki 0744033555
 
Aisee wezi wamechachamaa ila kuna namna mama alitoa namba za siri bila yeye kujua au laini ilikua mpya namba zake za siri "0000" ????
Unajua hizi smart phone Mara nying zinaweka mambo hadharani bila sisi wenyew kujua. Kupitia Keyboard za simu, zina tabia ya ku-save maneno tunayotumia Mara kwa mara, zinasave hadi password muhimu.
Usikute jamaa katumia mwanya huo kukomba salio.
Tuwe makini ... Mitano Tena
 
Kuna namba zasiri ambazo ni common mfano umri wa kuzaliwa mtu akichukeki tuuu akabuni mfano 1987 au anageuza 8719...kuna 1000,,, 2000,,,2580,,,,1234.
 
Mama asijifanye kuzuga zuga. Kuna jambo la siri aliongea na huyo mpambanaji.

Mi mwenyewe niliwahi pigwa na mtu kwa sim banking laki 2 na 30, nikafanikiwa kuokoa laki 2.

30 ikaenda lakini nikamshika hawara wa mwizi wangu baada ya miezi mitatu.

Aende polisi aripoti hio namba iliopigwa kisha kitaeleweka.

Kama uko Dar nicheki 0744033555
Nilikuwepo hapo hayo yote yakiendelea. Alitoa simu akampa, yule Kaka akajifanya anapiga then akasema haupatikani akarudisha Simu. Akashuka akisema anaenda maramoja kununua vocha. Asante ntakucheck
 
Nilikuwepo hapo hayo yote yakiendelea. Alitoa simu akampa, yule Kaka akajifanya anapiga then akasema haupatikani akarudisha Simu. Akashuka akisema anaenda maramoja kununua vocha. Asante ntakucheck
Cha muhimu uje namba iliopigwa

Nakuunga na makamanda wa cyber crime
 
Mama asijifanye kuzuga zuga. Kuna jambo la siri aliongea na huyo mpambanaji.

Mi mwenyewe niliwahi pigwa na mtu kwa sim banking laki 2 na 30, nikafanikiwa kuokoa laki 2.

30 ikaenda lakini nikamshika hawara wa mwizi wangu baada ya miezi mitatu.

Aende polisi aripoti hio namba iliopigwa kisha kitaeleweka.

Kama uko Dar nicheki 0744033555
Mkuu hebu ongeza nyama kwenye huu mkasa wako maana inaonekana kuna kitu cha kujifunza hapa.
 
Back
Top Bottom