Utapeli huu umemkuta mwenzetu.
Ndugu wapendwa,
>
> Story ifuatayo ni ya kweli maana imenitokea mimi
> binafsi jana tarehe 11/11/2009. Najua kwa kiasi fulani
> itakuwa inaninizalilisha kwa kutokuwa makini lakini naona ni
> vyema niwashirikishe rafiki zangu ili msije
> mkatapeliwa kama mimi na wengine wengi wameshatapeliwa
> kama vile ndugu yake Galeba, laiti Galeba angeweza
> kutuelezea yaliyomsibu ndugu yake labda na mimi ningeweza
> kuepuka utapeli huu. Kinchosikitisha matapeli wenyewe ni
> watu wanaotufahamu vizuri.
>
> Mnamo muda wa saa tano asubuhi nikiwa nyumbani (nipo
> likizo) nikapokea simu nisiyoifahamu kutoka kwa mtu ambaye
> alijitambulisha ananifahamu, na kwa jinsi alivyonitaja kwa
> jina na career background details zangu sikuwa na
> shaka kwamba hanifahamu. Mazungumzo yalikuwa kama
> ifuatavyo:
>
> TAPELI: Mr. Alex Matovu habari za siku nyingi.
> Mimi: Nzuri
>
> Tapeli: Vipi bado unafanya kazi Blue Financial Services?
> Mimi: Hapana, nani mwenzangu?
> Tapeli: John, nilikuwa nafanya kazi Wizara ya elimu, na
> uliwahi kunisaidia nikapata mkopo, ila kwa sasa nipo World
> food programme, Kigoma kama Chief supplies officer.
> Mimi: okay sasa nikusaidie nini John (ukweli nikwamba
> sikumkumbuka ila kwa kuwa tulikuwa tunatoa mikopo kwa
> wafanyakazi wa serikali, siku jiuliza sana, after all
> alikuwa hajasema anachotaka)
>
> Tapeli: Sasa nina issue naomba unisikilize kwa makini, kama
> unavyofahamu WFP tunatoamisaada ya vyakula hivyo tuna
> maghala makubwa ya kuhifaadhi chakula, hivyo ili kuhakikisha
> vyakula haviharibiki huwa tuna weka presavative inayoitwa
> Damoline Liquid solution made in Sweeden, hii inapatikana
> MSD na kwa licensed dealers kama Mohamedi Enterprises.
> Kwahiyo tuli float tender mwaka jana na supplier aliyeshinda
> tulikubaliana anipe 10% lakini baada ya ku supply hayo
> madawa akanidhulumu na
> kunitisha kuwa iwapo nitamdai hiyo 10% angeniripoti kwa
> mabosi wangu. Kwa hiyo sikuwa na cha kumfanya bali kusubiri
> contract yake iishe alafu nimtafute supplier mwingine. Sasa
> ndio nikaona nikupigie ndugu yangu maana nakujua wewe hii
> kazi utaweza kuifanya ukizingatia unalipwa cash on
> delivery!
>
> NOTE: nimeshawahi ku deal na supplies officer wengi
> hivyo sikuwa na doubt yeyote, bali nikaona hii is just
> another deal kama ambazo nimeshawahi kufanya
> successfully.
>
> Mimi: Okay sasa unataka nifanye je?
>
> Tapeli: Unachotakiwa kufanya ni kwenda MSD umuone Dr.
> Shija, huyu ndiye mkuu wa hapo na ndiye aliyekuwa supplier
> wetu wa zamani aliye ni dhulumu, sasa kwa kuwa sitaki kumpa
> kazi tena, wewe uende ujifanye unaulizia hiyo liquid
> solution, na u negotiate ujue atakuuzia shillingi ngapi.
> Kwahiyo nakutumia simu yake mpigie muongee akupe quotation,
> alafu akisha kupa bei nipigie ili nikuelekeze cha kufanya.
>
> Basi
> wandugu nikampigia dr. shija, mwanzoni shija ana hesitate
> kuzungumza na mimi aki pretend kuwa hapendi kuongea na
> strangers na akataka kujua namba yake nimeipataje, sasa kwa
> kuwa siwezi kumwambia ukweli kuhusu aliyenipa namba yake,
> ikabidi na mimi niwe muongo kwa muda, nika pretend kuwa mimi
> ni mkulima na nahitaji hiyo presavative kwa ajili ya maghala
> yangu yaliyopo arusha. Basi akawa na imani na kukiri kuwa
> anayo stock yakutosha, na hiyo liquid inauzwa kwa pair ya
> chupa mbili zenye ujazo wa 1000mls, kila pair ni 1.2m. Sasa
> angalia nilivyoingia katika mtego, baada ya kunipa bei ni
> kaomba punguzo na akasema atauza kwa 1million.
>
> Nikafanya kama nilivyoelekezwa na John wa WFP kuwa baada ya
> kupata bei nimjulishe nilivyomjulisha akasema kinachofuata
> ni kuwa mimi nitauza kwa USD. 1700, na tofauti kwa
> maana ya faida tutagawana, hivyo nisubiri aniunganishe
> kwa bosi wake for further final details.
>
> Basi wandugu kama mnavyonijua
> katika issue za fwedha, nikachukua calculator ya simu ili
> nijue deal ina shillingi ngapi, hela zilivyokuwa nyingi hata
> calculator iligoma, maana WFP wanahitaji 50 pairs @ usd
> 1700, mimi nanunua kila pair kwa 1million ambayo ni kama usd
> 770 hivyo difference usd 930 x 50 pairs = USD 46500, ALAFU
> tunagawana pasu pasu. Guys you can imagine what was going on
> in my head!
>
> Basi kweli muda si mrefu nikapigiwa simu na huyo bosi wake
> ambaye ni mzungu na mazungumzo yalikua kama ifuatavyo:
>
> MZUNGU: This is Mr. Scheinder from WFP, are you the new
> supplier?
> MIMI: YES
> MZUNGU: Do you have enough stock of Damoline Liquid
> solution; we are looking for 50 pairs?
> MIMI: Yes I have sufficeint stock
> Mzungu: what is your price per pair?
> Mimi:$1700
> Mzungu: ahaaaaaaaa thats a very good price, do you want to
> be paid in dollars or TZS
> MIMI: Dollar of course, you how how unstable the local
> currency is ( Hapo tena na mimi nataka kuonyesha
> kuwa ni International businessman)
> Mzungu: No problem, we have enough dollars, you want to be
> paid cash or by cheque?
> Mimi:Cash
> Mzungu: Okay no problem, now listen very carefully mr. new
> supplier we need this liquid urgently possibly today, and
> since you have said you have enough
> stock we are taking off this morning from Kigoma coming to
> Dar, please arrange for the transport to take us to
> Movenpick, we will pay usd. 200 for your fuel, but most
> importantly make sure you bring one pair of the sample with
> you.
> Mimi: No problem at all I have been in this business for
> quite sometime now you can be sure everthing will be fine.
>
> Masikini bila kujua nimeingizwa kingi, nikachukua cheque
> book, nikaandika cash withdraw 1million ili nikanunue sample
> yakwenda kuwaonyesha wateja wangu. Baada ya kutoka bank
> nikampigia dr. shija ili aniuzie hiyo sample, akasema kwa
> sasa ametoka ofisini ila sample anazo katika gari na alikuwa
> anaelekea
> Mwananyamala hosp, then Magomeni alafu Muhimbili, hivyo
> tukutane Magomeni hosp. Yaani jinsi nilivykuwa naendesha
> gari basi hata kama ni mashindano ningeweza kushinda, basi
> mimi mbio mpaka magomeni hosp namsubiri dr. shija.
> Nikampigia akasema yupo ndani hospitalini na yupo na mabosi
> wake asingeweza kutoka ila anamtuma kijana wake nimpe hizo
> fedha na yeye anipe hizo dawa, kweli ikawa hivyo kijana
> akaja akaingia kwenye gari nikamwambie anipe hizo sample
> kwanza nikazisoma ziko exactly kama WFP wanavyotaka!
> NIKAKABIDHI HELA 1 MILLION. Bila hata aibu yule kijana
> akaniomba 50,000/= nikamwambie asijali maana deal kubwa
> itakamilishwa saa nane.
>
> Kwa kuwa wageni wangu walishaniambia niwaaandalie usafiri,
> nikampigia dreva tax wangu aje airport saa nane, nikamuuliza
> bei kutoka airport mpaka movenpick ni ngapi akasema 25,000
> nikamwambia usijali ntakupa 50,000/=!!!!!!!!!!!!! (Kumbuka
> mimi ntalipwa usd 200 ya usafiri).
>
> Basi mimi mbio nikaenda
> airport terminal one kusubiri ndege ya WFP ili tumalize
> biashara, nilipofika kuulizia reception nikaambiwa hakuna
> kitu cha namna hiyo na mimi ni mtu wa 10 kutapeliwa, basi
> tena nikajirudia kimya kimya. Nikaenda kula chefs pride
> nikamsimulia jamaa mmoja yaliyonisibu, kabla sijamaliza
> akasema hata ndugu yake ametapeliwa wiki iliyopita,
> nikampigia Galeba akasema yeye jamaa yake alipigwa 3.5m last
> week.
>
> Taarifa nilizonazo mpaka nikuwa hii ni network ya wahaya na
> mpaka sasa ni wahaya wengi wameishaibiwa ukilinganisha na
> makabila mengine.
>
> So guys thats my story for yesterday!