marksalewi
Member
- Apr 7, 2012
- 96
- 25
- Thread starter
- #21
Leo mchana nilitembelea kwenye ukurasa wangu wa facebook nikaona Mh. Zitto Kabwe ameandika kwenye ukurasa wake kuwa mikopo ya vikoba itawasaidia Watanzania wengi na kumhusisha mh. Rais kuwa ametoa pesa kwa ajili ya kuwasaidia wajasilia mali wadogo wadogo. Pia wameonesha mh. Lowassa akifungua taasisi hiyo katika picha kwenye magazeti ya habari leo na uhuru.
Nimetuma pesa sh. 500,000/- baadaye kidogo wakanipigia kuwa wameipata wanashughulikia mkopo wangu. Aliyepiga kwanza ni mwanaume. Baada ya kama nusu saa akapiga msichana Akaniambia natakiwa nitume 105000/- kwa ajili ya kiingilio kwenye hiyo saccos na mkopo wangu upo tayari na kuwa niitume ili wanitumie huokopo.
Ikumbukwe masharti ya mkopo yalikuwa ni kiasi utakachoweka kama dhamana utapewa mara kumi yake. Na ni kuanzia 500,000/- mpaka 1,000,000/-. Niliwaamini kwa vile Niliona viongozi wakubwa katika nchi hii wamehusika na pia magazeti ya chama na serikali yameonesha mh. Lowasa akifungua hiyo taasisi.
Wamerudi kama nilivyowahi kuleza hapo. Mwenye kuweza kuwasaidia watz afanye hivyo jamani.