Utapeli mpya kupitia sms

Utapeli mpya kupitia sms

Kisendi

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2009
Posts
699
Reaction score
180
Ndugu wana JF kuna utapeli mpya umeibuka kupitia sms. Hii imemutokea rafiki yangu hapa ofisini.

Kuna mtu amekuwa akimsumbua kumpigia simu kila siku!! Kufikia jana jioni akwambie mimi naitwa xyz naomba usinisumbue kama unataka kuhakikisha jina langu tuma kwenye hii namba yangu hata 500 ili uone jina langu. Baada ya muda mfupi ujumbe ukaangia kwenye simu yake. Unasema umepokea Kiasi cha Tsh.10000 kutoka kwa (JINA LA MSANII). Jamaa akahamaki na kuamua kumpigia simu huyo bwana akimwambia mbona umetuma hela nyingi hivyo jamaa akasema nilitaka kuangalia jina. Kweli ni wewe nirudishie hiyo pesa. Baada ya hapo jamaa aliyetumiwa pesa akaangalia salio ili airudishe akaona hamna kitu. Kurudi kuisoma hiyo sms iliyoingia kumbe kaituma yeye mwenyewe na sio kwenye kampuni ya simu lakini huo ujumbe umetengenezwa kama umetoka kwa -PESA!! Kwa hiyo kama jamaa yangu angekuwa na salio angeweza kutuma na mwisho wa siku angejikuta ametapeliwa.

UKIONA DALILI KAMA HIZI CHUKUA TAHADHARI.
 
Hata kama ingekuwa ni pesa kweli mimi nisingerudisha, si ametuma mwenyewe kwa uchizi wake. Huo ni wizi wa kishamba, ila shukrani kwako mleta uzi kwa taarifa.
 
Duuuuh matapeli nooma aisee yaani hawachoki ni mwendo wa kubuni njia mpya za kuwaibia watu....ahsante kwa taarifa
 
Hivi nyie wamasai. wakurya na wahaya mtaendelea kutapeliwa kkitoto hadi lini ? mnaboa kwa ujinga.
 
Ndugu wana JF kuna utapeli mpya umeibuka kupitia sms. Hii imemutokea rafiki yangu hapa ofisini.

Kuna mtu amekuwa akimsumbua kumpigia simu kila siku!! Kufikia jana jioni akwambie mimi naitwa xyz naomba usinisumbue kama unataka kuhakikisha jina langu tuma kwenye hii namba yangu hata 500 ili uone jina langu. Baada ya muda mfupi ujumbe ukaangia kwenye simu yake. Unasema umepokea Kiasi cha Tsh.10000 kutoka kwa (JINA LA MSANII). Jamaa akahamaki na kuamua kumpigia simu huyo bwana akimwambia mbona umetuma hela nyingi hivyo jamaa akasema nilitaka kuangalia jina. Kweli ni wewe nirudishie hiyo pesa. Baada ya hapo jamaa aliyetumiwa pesa akaangalia salio ili airudishe akaona hamna kitu. Kurudi kuisoma hiyo sms iliyoingia kumbe kaituma yeye mwenyewe na sio kwenye kampuni ya simu lakini huo ujumbe umetengenezwa kama umetoka kwa -PESA!! Kwa hiyo kama jamaa yangu angekuwa na salio angeweza kutuma na mwisho wa siku angejikuta ametapeliwa.

UKIONA DALILI KAMA HIZI CHUKUA TAHADHARI.

Kuna ndugu yangu aliibiwa simu wiki iliyopita pale Mwenge. Kesho yake mwizi kwa kutumia simu ya wizi kamtumia mdogo wangu mwingine ambaye alipata namba yake kwenye simu aliyoiba kwamba "naomba uniazime laki moja nitakurudishia kesho kama saa sita mchana ila nitumie kwenye namba yangu ya tigo na........ naana Mpesa nimesahau password". Hakujua kwamba huyo anayemdanganya yupo na huyo aliyeibiwa simu. Basi mdogo wangu kapotezea kama kwa saa mbili hivi kisha kamtumia text mwizi kwamba alitaka kumtumitia laki tano yake aliyokuwa anamdai ila hela ipo kwenye simu ya voda na hana salio la kutumia, naomba amtumie vocha ya elfu tano ili amtumie voda kwa tigo. Lol!! Mwizi haraka katuma vocha ya elfu tano ya voda bila kujua amepunguza kwenye bei ya simu ya tochi aliyoiba. Baada ya hapo mwenye kuibiwa simu kaenda kublock sim card yake.!!!!!
 
tatizo la ajira tanzania ni bomu lililolipuka tayari na haya ndo madhara yake tunayapata na tutegemee madhara makubwa zaidi na zaidi.
 
hii wanaibiwa washamba kama nyie...wajanja ukitutumia hiyo hela akirudi kitu maana riziki haivutwi kwa kamba
 
huyu ndo tapeli wa kwanza mshamba kumuskia,........haha angetapeliwa najua kwa aibu asingekusimulia...ila shukurani kwa taarifa:flypig:
 
Kwani ili ujue jina la mtu kupitia hizo ....-PESA ni lazima utume hela? Mimi nijuavyo kutuma hela ni hatua ya mwisho baada ya kujua jina la unaemtumia.
 
Back
Top Bottom