Utapeli kwa mawakala unakuwa hivi!

Utapeli kwa mawakala unakuwa hivi!

Adil_101

Senior Member
Joined
Jul 26, 2022
Posts
110
Reaction score
345
Habari za Asubuhi Wakubwa!!

Leo nimeamua kuwa changamsha kidogo na mada ya utapeli especially kwa mawakala jinsi utavyofanyika.

Huwa inakuwagaa hivi

Anakuja dukani Mtu Mzima fulani hivi alievaa mavazi ya official wengi wanavaa suti, tai na miwani.

Akija dukani anakuwa akizungumza na simu na huenda akaletwa na Tax au Private Car.

Mazungumzo ya hawa matapeli yanakuwa smart sana...

Like "Alfred unajua ule mradi niliamua mpewe nyie vijana wangu sababu napenda kuona mnakua kiuchumi" hapo hapo unashangaa anaongea na simu nyingine like...

"Hello Catherine, i will check u back" halafu baada ya hapo unaskia Habari Kijana huku akitabasamu na simu kaishikilia..

Kama vile bado anaongea, Utaskia "Samahani mna huduma ya TIGO PESA hapa?" halafu unaskia "Sorry Alfred acha nimuwekee Kanjunju John pesa yake ya Transport then nitakupigia".

Sasa bwana kuanzia hapo sasa anakuwa ameshakuteka psychology na unakuwa huna mashaka nae kabisa 🥲...

Bwana bwana bwana!!! Muvi la kutisha linaanza sasa. Kwanza ndugu tapeli anakuuliza "Milioni 1 si napata eeh".

Jibu lako either liwe ngoja niangalie au ipo basi yeye anakupa mzigo anakwambia hesabu.

Hapo unapewa milioni yenyewe imekamilika kabisaaa au hata anaweza kuzidisha..

Maumivu yanapoanzia sasa wakati wewe unamalizia kuhesabu Ndugu Mheshimiwa Tapeli atapokea simu au atajifanya anampigia mtu simu sasa utaskia...

"Hello Bajabir hii fedha nikuwekee kwa namba gani? Pleas be on time my friend Msafara unakabiria"

Wakati huo unachotakiwa uelewe..

Ni kuwa huyu Mheshimiwa Tapeli anakuwa ameshakuchora muda sana, ameshajua hauna CCTV, ameshajua weakness zako na mzunguko wako wa Wateja upoje.

Hawaendi sehemu yenye msongamano mkubwa.

Baada ya kuzuga anaongea na simu atakwambia either "Sorry naona huyu simuelewi"..

Inaonekana hajakuwa tayari na unaweza kumuwekea pesa akaja kusema hajaona na mimi nitakuwa nishaondoka".

Sasa bhana wewe ukimkabidhi hizo pesa tu kuna sekunde 2 kama sio 3 anakuzuga kidogo hv anabadilisha pesa kwenye koti la suti ila wewe ukiendelea kumtizama unaona...

Bado kazishikilia zile zile fedha.

Sasa hapo utaskia anakwambia tena "Au tufanye hv kwanini usitume kwangu kisha nikamtumia nikiwa safarini huko huko?" Atacheka halafu atajichekesha na wewe utajaa utazugwa na tabasamu atakwambia "okay naweza kukutajia No. Sasa eeh"

Wakati huo.

Sasa wewe umeshika simu ndugu yangu utashikishwa pesa huku unatuma .
Wakati unakaribia kutuma atakwambia jina fulani ile umeweka namba ya siri tu yeye huyooooooo anapotea"

Hapo sasa kinakujia kile kiakili cha "Kuthibitisha tena pesa ili uzigawe either au uweke kwenye droo.

Ndugu yangu katika Upendo wa Bwana Mungu wetu utahisi kwanza ganzi maana kuna mambo hutayaelewa ile unarudi sasa kwenye akili yako unaangalia chini na juu unaona 2000 kibaoooooo.

Ile unahamaki ndugu Mheshimiwa Tapeli anakuwa hayupo tena area yako. Ila unasema upige simu..

HQ utaambiwa hii No. Imetumiwa 1,000,000 kweli ila hii pesa imeshatolewa hivyo hakuna namna ya kukusaidia tena labda uende Polisi kwa hatua zaidi.

Wakati huo Mkononi una kama 150k tu.

Ndugu zangu haya mambo yapo na wala hayamkuti Mjinga, Ni kuomba Mungu tu.

END
 
Adil ahsante kwa uzi mzuri, kwa kweli wanaosema matapeli wanatumia dawa wala sio kweli wale jamaa wana trainings zao kabisa, yaan kujikwamua nao ni kumuomba sana Mungu,
Umetufumbua wengi macho.
 
Hii ilitokea dukani mke wangu ndio alikua anahudumia. Kuna 1m nilikua nayo kwenye simu nikasema ngoja nitoe then nikifika town nimpe namba ya wakala mwingine aitoe.
N:B mke alikua mgeni kwenye uwakala nilijua atapigwa tu ili apate akili so nilikua naacha mtaji less than 400k, siku hiyo bana wakaotea na mbinu hiyo. Alipigwa kama laki 7
 
Hii ilitokea dukani mke wangu ndio alikua anahudumia. Kuna 1m nilikua nayo kwenye simu nikasema ngoja nitoe then nikifika town nimpe namba ya wakala mwingine aitoe.
N:B mke alikua mgeni kwenye uwakala nilijua atapigwa tu ili apate akili so nilikua naacha mtaji less than 400k, siku hiyo bana wakaotea na mbinu hiyo. Alipigwa kama laki 7
Wanawake ndiyo wahanga wakuu wa matapeli kwenye biashara ya miamala, kutokana na mioyo yao kuwa myepesi kwenye kuamini kila wanacho ambiwa na hao matapeli.

Bila shaka ukiwa na cct camera pamoja na money counter machine; vinaweza kudaidia kupunguza aiana hii ya utaleli.
 
Sikuzote mtu tapeli ana akili ya ujanja ujanja... Thinking capacity inakua juu... Ndio maana mtu yoyote anaweza kutapeliwa ktk mazingira haya au yale... Ningekua sina kazi ya kueleweka ningekua tapeli, maana ni kazi ambayo ni ngumu kukamatwa na ukikamatwa huitiwi mwizi (maana muonekano sio wa mwizi) zaidi ya kushikwa na kupeleka police na ukifika police kesi yake huwa haielewek hivyo mnaishia kukubaliana mtalipana vipi...
 
Mambo haya yaepuke ukiwa una dili na mambo ya pesa nyingi (ukiwa unanunua kitu kwa pesa nyingi kama nyumba , Gari kiwanja n.k)
Usinunue kwa influence ya watu walikuzunguka kwa kuzingatia maneno yao tuu bila udadisi
Usijarbu kufanya biashara yako nje ya utaratbu
Epuka biashara zenye kujaa wapambe ambako wengi huwajui/madalali
Mzingatie mshauri wako wa Kibashara na huku ukiwa Tayar ulikuw na taarfa za awali mapema kbsa
Sio ununue kwa haraka sana ukizan utakosa nenda katazame kaaa dadisi ata kwa siku 3 then nunu wakat wote usijinyoshe umekipenda sana au wew tulia itakusaidia ata wao kama wanauza bei juu watakupunguzia
 
Mambo haya yaepuke ukiwa una dili na mambo ya pesa nyingi (ukiwa unanunua kitu kwa pesa nyingi kama nyumba , Gari kiwanja n.k)
Usinunue kwa influence ya watu walikuzunguka kwa kuzingatia maneno yao tuu bila udadisi
Usijarbu kufanya biashara yako nje ya utaratbu
Epuka biashara zenye kujaa wapambe ambako wengi huwajui/madalali
Mzingatie mshauri wako wa Kibashara na huku ukiwa Tayar ulikuw na taarfa za awali mapema kbsa
hakika mkuu
 
Adil ahsante kwa uzi mzuri, kwa kweli wanaosema matapeli wanatumia dawa wala sio kweli wale jamaa wana trainings zao kabisa, yaan kujikwamua nao ni kumuomba sana Mungu,
Umetufumbua wengi macho.
Tuko Pamoja Mkuu
 
Kusema kweli mimi nikiona mtu kavaa suti na tai huwa na kaaga mbali nae...halafu na mtazama tu!

Kwasababu nakumbuka kipindi hiko nipo sekondari nasoma tuliwahi panda kwenye daladala (mimi na Bi mkubwa) na Mtu ambaye alivaa ki-official, bila ya kujua kama jamaa alikuwa mwizi....

Wakati tunakaribishia jamaa alikwapu simu ya bi mkubwa kwenye mkoba bila ya maza kujua na akajitia "wee konda niache hapo"

....na dakk 10 mbele maza anashtuka kuwa tayari wameshamliza

....yaan toka siku hiyo mimi nikimuona mtu kavaa suti na tai alafu anajifanya ni mtu mzito huwa na kaaga mbali nae yaan sitaki anitongoze na maneno au muonekano wake kabisaa!
 
Back
Top Bottom