Kuna utapeli unaendelea kufanyika katika uuzaji wa maeneo kwa kushirikiana baina ya wauzaji, madalali na serikali za mitaa ambazo zimekosa uadilifu. Mnaonunua maeneo mitaa ya Goba, Kinyerezi, Kibamba, n.k kuweni makini sana. Leo nimeshuhudia ndugu mmoja alikuwa anataka kuuziwa kiwanja huko Goba na jamaa mmoja akisema ni shamba la mkewe lakini jamaa na baadhi ya watendaji wa serikali ya mtaa wakiwepo wakati wakijua wazi kuwa eneo lile lina utata...