• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Utapeli huu kwa wanaouza vitu....

ngoshwe

ngoshwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2009
Messages
4,141
Points
1,250
ngoshwe

ngoshwe

JF-Expert Member
Joined Mar 31, 2009
4,141 1,250
Leo nimesikia kisa cha tatu kinachofanana cha watanzania wenzetu kuibiwa kwa staili inayofanana...


Unapotaka kuuza kitu chako unatafuta njia muafaka ya kuwafikia wateja. Unatoa tangazo liwe kwenye gazeti, mtandao au bandiko kwenye mali au sehemu nyingine. Kuna matapeli wanakupigia, unaongea na mtu ambaye kwa sauti huwezi kudhania ni "mhuni", unasikia sauti ya mzee wa makamo tu kuwa anahitaji hiyo mali. Kama ni gari, kwa wale waliokumbwa na mkasa huo wanasema jamaa anakuambia yeye yupo mbali Kama upo Dar anasema yeye yupo Moshi. Mwanza nk anafanya bisahara, ila atatuma vijana/kijana wake waje/aje kuiangalia gari . Mara nyingi hasiti kukubali bei. Baada ya muda mtu mwengine utapigia simu na kujitambulisha kuwa ametumwa na mzee (Yule uliyeongea nae kabla) na kukuambia kuwa yupo mitaa fulani ila amuelekeze sehemu unayoona inafaa na usalama ili muonane aweze kulikagua gari.

Unaweza kuchukua tahadhari zote, labda utakuwa na mtu wako, ukienda kuonana nae mlipopanga atakagua gari na kusema lipo njema ngoja awasiliana na "mzee".

Unaweza kumpa muda, baadae atakutafuta kama sio hapo hapo, atasema mzee yupo tayari amefurahi. Ila umpe maelekezo ya jinsi ya kulipia na angependa kulipa mapema. Kwa tahadhari unaweza kumweleza kuwa tukalipie Benki, kama sio yeye kukuambia ni vizuri ikiwa Benki. Atajifanya anacheki na "Mzee" kisha atasema sawa na itahitaji kuandikishana kwa wakili pia kwa kuwa dunia imebadilika.

Mtakubaliana ili aweze kulipia Benki, katika kipindi hicho ambapo unatarajia "hela" anaweza kukuzungusha akili kwa kukuambia aongee tena na mzee kupata maelekezo ya jinsi ya kutuma hela..baada ya muda atakuambia kuwa Mzee anasema atatuma hela kupitia benki fulani ambapo kuna mtu hapo (mtumishi wa Benki au ndugu mwingine) ili muende kumfuata awape hela ili yeye akaziweke (deposit) kwenye Benki yako na akupe "Pay Slip" . Ukikubali hapo ndipo umeliwa , kama una simu nzuri, hela au Laptop, mkifika karibu na eneo la karibu na hiyo Benki ambayo anakuadaa muende akachukue hela, atakuambia, hebu subiri nimpigie jamaa, kisha atashuka kwenye gari kama mlikuwa pamoja..kisha atarejea tena na sound, "duh, simu imekata vocha" nipa ya kwako na atakaa kwenye gari huku akiitumia ili kukuzuga. Au hata kama hamkuwa kwenye gari moja, atakufuata, atakuomba akae kwenye gari yako ili kumsubiri jamaa, baada ya muda atajifanya anampigia simu, kisha atasema vocha imesha mkuu ebu nipe yako mara moja, atakuomba wewe umpe simu yako (huwezi kufikiri atakuibia kwa kuwa mpo pamoja kwenye gari na kwamba kama ni kukuibia, wewe "attention" yako inakuwa ni kwenye gari tu na sio vitu vingine ) , ukimpa atajifanya akimwelekeza jamaa kwenye simu... " Kakaaa...toka nje. basi faster""??....na kukutaka wewe usogeze gari karibu na hiyo Benki ili jamaa akitoa aweze kupokea hela haraka.wananchi wasione.......Huwezi kumdhania vinbaya, lakini hapo ndio utakuwa "umebugi meen", ukiwasha gari na kuanza kutembea, atakuzuga nenda taratibu, ngoja, ngoja, hapo anajifanya anaongea na jamaa (ehhee upo hapo, toka basi, gari ni aina ya ....rangi..check hapo, wapi....ebwana haraka mkuuu...ebu...atajifanya anataka kuchungulia nje...kisha atashuka kwa kasi akiwa na simu yako na laptop (Kama unavyo) ...ina hii inaweza kuwa sehemu ya kadamnasi kubwa kama Kariakooo huwezi kumfuata au kupiga kelele....

Kama hatafanikiwa hapo kukutega siku hiyo ,atatafuta tu mwanya...ukiona umezubaa atakuelekeza maeneo ambayo ukiwa unahangaika kutafuta "parking" yeye ataondoka na simu au laptop kirahini mkiwa wote....kama ataona u mjanja fulani, anaweza kuku trick, kuwa deal msitishe ili lifanyike kesho, ataendelea kukufuatilia hivyo hivyo mpaka siku ambayo upo peke yako, atakubabatiza tu ili akuibie..

CHUKUENI TAHADHARI MNAPO UZA MALI ZENU
 
kbm

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Messages
5,141
Points
1,500
kbm

kbm

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2012
5,141 1,500
Duh! Mjini shule. Asante kwa kutujuza. JF ni kila kitu.
 
Nivea

Nivea

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2012
Messages
7,459
Points
1,250
Nivea

Nivea

JF-Expert Member
Joined May 21, 2012
7,459 1,250
Haibiwi mtu hapa leo tu kuna jamaa alikuwa na pesa yangu kitambo leo imebidi nimmpelekee wahuni ile wamemwinamisha kula mzigo akatoa hela yangu yote nikasepa nanii mwaka sasa lol nimecheka sana leo
 
ngoshwe

ngoshwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2009
Messages
4,141
Points
1,250
ngoshwe

ngoshwe

JF-Expert Member
Joined Mar 31, 2009
4,141 1,250
Haibiwi mtu hapa leo tu kuna jamaa alikuwa na pesa yangu kitambo leo imebidi nimmpelekee wahuni ile wamemwinamisha kula mzigo akatoa hela yangu yote nikasepa nanii mwaka sasa lol nimecheka sana leo
Huwezi kung'amua mara moja mkuu. Huyo aliyekuwa na hela yako akairejesha baada ya kumfanyia uhuni ni tofauti na mtandao tunaoelezea.
 

Forum statistics

Threads 1,405,596
Members 532,052
Posts 34,490,138
Top