Utapeli bado unaendelea

proxy

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2016
Posts
1,481
Reaction score
1,356
Leo asubuhi sana nimeamushwa na ujumbe huu kutoka namba 062953411* bila shaka hii ni namba ya Hallotel, ombi langu kwa Kampuni ya Hallotel ni kwamba watoe ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama ili kuwabaini hawa watu wanaoharibu taswira ya kampuni yao

"Hongera!!!
Namba yako imechaguliwa kushinda Tsh10,000,000 katika droo ya JUMATAMU JENGA na BIKO.Ili uweze kutangazwa mshindi unatakiwa ulipie UPFRONT FEE (ADA YA UTANGULIZI) ambayo ni bima ya ushindi wako asilimia 0.53% sawa na Tsh53,000 kupitia namba 065361775* kisha utapigiwa simu ukiwa umeunganishwa na vyombo vya habari kuutangazia umma ushindi wako.
LIPA MAPEMA ILI USIPOTEZE NAFASI YA USHINDI
BIKO Mshiko Nje! Nje!
UJUMBE HUU NI SIRI,USIUTOE HADHARANI"
 
Nimeipenda hii...."UJUMBE HUU NI SIRI, USIUTOE HADHARANI"...

Sasa wewe umeshaharibu kuutoa hadharani. Hapo haupewi tena mil 10.
 
Walianza wale wa " ile pesa tuma ktk namba hii. Simu yangu ina shida". Sasa wamekuja na njia nyingine.
 
Haya bhana maana nimeishia kucheka tu,ila umevunja masharti mkuu kwa kutoa siri hapa
 
Alafu hiyo namba mwenye nayo anaitwa hadija kama sijakosea hata juzi kunabmtu katumiwa hiyo msg tukaicheki ikaja jina hilo
 
Mkuu unakuta kuna mtu ameibiwa simu halaf hao jamaa walioiba wanatuma msg kwenye majina yote yaliyoseviwa kwenye simu mkuu.

Sasa utakuta kuna baadhi ya watu wanatumiwa hawaijui namba yako aidha mliwasiliana mara moja tu au baada ya kununua line nyingine ukasevu namba zao au ulipata namba baada ya kuweka line mpya na kuzipata kutoka gmail.

Kwa hiyo wengine wanapatwa na hilo tatizo aisee kwa hiyo kiuhalisia sio wao wanaotuma hizo msg ila ni namba yake imetumika aidha baada ya kupoteza au kuibiwa simu mkuu.

Ahsante.
 
Da mod hiyo namba umeamua kuificha kidogo ,lakini nilitaka iwe kama ilivyo ili hawa watu wajifunze.
 
Bila kificho kuna uhusiano mkubwa kati ya hawa matapeli na mitandao ya simu.
 
ni kweli mkuu na ndio maana tunatakiwa punde ukigundua umeibiwa, umepoteza simu utoe taarifa polisi kisha uende kwenye ofisi za mtandao unaotumia kuifunga simcard. pia ni muhimu kuweka password kwenye simu maana hatujui siku wala saa ya kuibiwa simu zetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…