Samahani mmeenda nje ya mada. Mimi nitaenda moja kwa moja kwenye point.
1. Kumbuka Asilimia kubwa ya watanzania ni wabantu. Kwa hiyo tumetokea kwenye jamii ya aina moja. Nakatika makabila ya kibantu yana dhana zifuatazo:-
a. Mashemeji kutania.
b. Babu na wajukuu. Na mengine mengi.
Katika kugawanyika kwa makabila ya kibantu yaligawanyika na dhana hiyo hiyo. Na makabila yote haya unayo yaona yametokana na koo mbalimbali. Kwa hii mantiki matani haya yote ni ya kihistoria.
2. Kuhusu nchi nyingine. Kwa uelewa wangu, kwa nchi za kibantu zinadesturi ileile. Lakini nchi ambazo si za wabantu si dhani kama wanautani huu. Maana mambo ya utani ni utamaduni wa kibantu, Katika kuelimisha, kukosoa, vilivile kuburudisha.