VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Mimi nimeusikia mahali utani huo. Sihusiki nao moja kwa moja. Wataniaji wanatania kuwa Rais aliyemaliza muda wake,yaani Rais Mstaafu, alikuwa mpenda safari na alikuwa akisafiri kweli mara kwa mara. Huyu wa sasa, wataniaji wanasema, anapenda kusifiwa. Unitaka usitumbuliwe,mwaga sifa.
Wataniaji wanasema kuwa kila hotuba za wakuu wa awamu ya nne ilikuwa na aya ya kusifu safari za nje za Rais. Kwa kutamka hivyo,teuzi hazikuwapitia mbali na hata usalama wa vyeo vyao ulikuwepo. Kwasasa, wanasema wataniaji,ukitaka usikilizwe bila kuchongewa,anza na sifa kwa Rais.
Ukishamsifia Rais hadharani,mambo yako yananyooka kama rula. Usipofanya hivyo kwa makusudi au bahati mbaya, utatumbuliwa. Wataniaji wanawataka Watumishi wanaotaka raha awamu hii kugharimia hata ukurasa gazetini au dakika redioni au luningani kumwaga sifa kwa Mkuu!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam