kalulukalunde
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 1,056
- 1,083
MOJA ya ajenda iliyobebwa na vyama vilivyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) katika kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka jana, ilikuwa ni kukosekana kwa mifumo katika sekta ya umma.
Hata hivyo, wabobezi wa masuala ya utumishi wa umma wanabainisha kuwa mifumo ipo, ila kinachokosekana huwa ni utashi wa kisiasa, utayari wa kiongozi mkuu kuisimamia mifumo hiyo ili iwe imara.
Utendaji wa Rais John Mgufuli, hususani hatua anazochukua katika kusimamia nidhamu na maadili ya utumishi wa umma, zinaelezwa kuwa msingi imara katika uimarishaji mifumo ya sekta za umma nchini.
Wanabainisha kuwa kama ni suala la mjadala basi iwe kwenye uimara wa mifumo iliyopo lakini sio kutokuwepo kwa mifumo. Mifumo husimamiwa na watendaji waliopo kwenye sekta ya umma, na kwa mujibu wa wataalamu hao ufanisi wao hutegemea zaidi nguvu iliyopo juu yao.
Wataalamu hao wanatumia mfano wa utaratibu wa kupima utendaji wa mtumishi kila mwaka kutokana na utumishi wake, ambao kwa kifupi hufahamika kama OPRAS, wanasema ukitumika vizuri unaweza kutatua tatizo la nidhamu na maadili katika utumishi wa umma.
Lakini pamoja na kuwepo kwa utaratibu huo wa OPRAS kwa miaka kadhaa sasa, bado haujaonyesha kuwa na mafanikio, sababu kuu ikitajwa kuwa ilikuwa kukosekana kwa utashi wa kiutumishi katika uongozi, hususani ngazi ya juu.
Katika kuhakikisha mifumo hiyo inakuwa imara, serikali kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani, USAID, imekuja na ufumbuzi kupitia Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma unaofahamika kwa kifupi kama PS3.
Mkurugenzi wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma, Dk. Emmanuel Malangalila, analibainisha jambo la msingi katika usimamizi wa mifumo kwenye sekta ya umma kuwa ni utashi wa kisiasa kwa kiongozi aliyepo madarakani.
“Mifumo ipo, jambo la msingi ni kuwepo kwa utashi wa kisiasa katika kusimamia mifumo hiyo,” anasema Dk. Malangalila katika mahojiano yake na Raia Mwema jijini Mbeya hivi karibuni.
Dk. Malangalila anasema kuwa ukiwepo utashi wa kisiasa na uwajibikaji katika ngazi zote za utumishi wa umma, kuanzia juu hadi chini, mifumo itaonekana kufanya kazi, tofauti na hali hiyo ni kutoonekana kwa mifumo ikifanya kazi.
Watalaamu hao wa masuala ya utumishi wa umma, wanaamini kuwa uwajibikaji wa viongozi ngazi za juu, ni msaada mkubwa sana kwa watendaji, kwamba huwapa ari ya kutekeleza majukumu yao na kuwamotisha.
Baadhi ya viongozi katika utumishi wa umma, waliohojiwa na mwandishi wa habari hii kuhusu mifumo ya sekta za umma, walisema kuwa miezi ya mwanzo ya utendaji wa Rais Dk. John Pombe Magufuli imethibitisha utashi wake katika kuona mifumo ikifanya kazi kwa ufanisi.
“Leo unaona kila mtumishi wa umma hataki utani kazini, ni kutokana na Rais aliyepo kutotaka masihara katika utumishi wa umma,” anasema kiongozi mmoja mkoani Mbeya ambaye hata hivyo aliomba kutotajwa jina lake gazetini.
Kutokana na utashi wa kisiasa ulionyeshwa na Rais Magufuli hadi sasa katika kutekeleza majukumu yake, wataalamu hao wanaamini kwamba, itasaidi kwa kiwango kikubwa kufanikiwa kwa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma, ambao uzinduzi wake umekuwa ukifanyika kimkoa.
Mradi wa PS3
Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma, kwa kifupi ukifahamika kama PS3 umeandaliwa kusaidia kuongeza ufanisi katika jitihada za serikali kuwahudumia wananchi wake.
“Mifumo ipo, mradi hauji na mifumo mipya,” anasema Dk. Malangalila.
Kwa mujibu wa nyaraka za mradi huo, PS3 imelenga kutoa msaada wa kitaalamu kwa serikali kuimarisha mifumo ya sekta za umma, kwa lengo la kusaidia kuimarisha ubora wa utoaji huduma za umma na matumizi yake, hususani kwa jamii za pembezoni.
Msaada huo wa kitaalamu ni pamoja na utoaji wa ushauri wa kitaalamu, kuwajengea wafanyakazi uwezo na kugharamia shughuli za mradi.
Sifa pekee ya mradi huo inaelezwa kuwa ni mfumo wake wa utekelezaji ambapo hufanya kazi kwenye sekta zote za umma huku kipaumbele chake kikiwa katika ngazi ya mkoa na halmashauri.
Mifumo ya sekta za umma inayohusika na mradi huo ni pamoja na utawala bora na ushirikishwaji wa raia, rasilimali watu, rasilimali fedha, mifumo ya mawasiliano na utafiti tendaji.
Mradi huo ni wa miaka mitano, 2015 hadi 2020, bajeti yake ikiwa ni dola za Kimarekani milioni 62. Mikoa 13 ya Tanzania Bara itanufaika na mradi huo kwa sekretarieti zake kupatiwa msaada wa kitaalamu ili ziweze kutekeleza majukumu yake.
Kutoka katika mikoa hiyo, Mradi wa PS3 utafanya kazi katika halmashauri zake zote 97 ambapo katika awamu ya kwanza zitachukuliwa halmashauri kutoka kila mkoa na awamu ya pili utazifikia halmashauri zote.
Halmashuri mbili za mwanzo kwa Mkoa wa Mbeya ni Chunya na Busokelo ambazo ziliteulliwa katika mchujo maalumu uliofanyika siku ya uzinduzi.
Pamoja na ngazi za mkoa na halmashauri, yapo mambo yanayotekelezwa pia katika ngazi ya taifa, ikiwemo majadiliano ya kisera na uimarishaji mifumo katika wizara, idara na taasisi mbali mbali.
Afya ni miongoni mwa sekta zilizopewa vipaumbele katika mradi huo, na tayari hati ya makubaliano imeshasainiwa.
Vikwazo kwa halmashauri nchini
Miongoni mwa changamoto zinazozikabili halmashauri nchini ni pamoja na ucheleweshaji wa fedha za miradi kutoka serikali kuu. Ushuhuda kutoka halmashauri mbali mbali nchini, zinabainisha kuwepo, mbali ya ucheleweshaji, pia utoaji wa fedha pungufu au kutotolewa kabisa.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kyela, Hunter Mwakifuna analitaja tatizo lingine linaathiri utendji katika halmashauri nchini ikiwemo Kyela kuwa ni utaratibu wa ajira ambao umesababisha nafasi nyingi kuwa wazi kutokana na ukiritimba katika mfumo wa ajira.
“Nafasi nyingi zipo wazi, hata nafasi za wahudumu tunalazimika kuomba tume ya ajira,” anasema Mwakifuna.
Afisa Serikali za Mitaa Mkoa wa Mbeya, Geofrey Anania anabainisha kuwepo kwa tatizo la mawasiliano kati ya serikali kuu na serikali za mitaa, hatua aliyosema inachangia kuathiri ufanisi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Kwa mujibu wa Anania, ufanisi katika mawasiliano ya serikali hizo mbili ni nguzo muhimu katika utoaji huduma kwa wananchi kupitia serikali za mitaa.
Mradi wa PS3 unatarajiwa kuondoa udhaifu ulipo kwenye mifumo ya sekta za umma, kwa kuongeza ufanisi kwenye utekelezaji.
Mathalani, Dk Malangalila anaungalia mfumo wa utawala bora ulipo kwamba unahitaji uwazi na uwajibikaji. Viashiria vyenye kuonyesha udhaifu katika mfumo huo hivi sasa ni pamoja na kamati za afya na elimu zilizopo, zinatakiwa zikutane, lakini hali halisi ni kwamba hazikutani.
Wananchi hawapati taarifa kama inavyobainishwa kwenye huo mfumo, hakuna ushirikishwaji wa wananchi katika mipango yao vijiji, badala yake kinachofanyika ni mtiririko wa maagizo toka juu kushuka chini.
“Katika hali hii ilitakiwa wahusika wawajibike, lakini haifanyiki,” anasema Anania.
Mradi huo unahakikisha kuwepo kwa kiungo kati ya serikali kuu na serikali za mitaa katika masuala ya kitaifa kama vile sera na miongozo.
Kupitia mradi huo inatarajiwa kwamba, masuala kama ya sheria zilizopitwa na wakati yanapofanyiwa marekebisho na taarifa zake kuwafikia wadau kwa wakati, pesa iliyopangwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo na huduma mbali mbali zinatolewa kwa wakati na kwa kiwango kilichopitishwa.
Matarajio ni makubwa kwa mradi huo, kwamba utawezesha kuimarishwa kwa mifumo ya sekta za umma, ikizingatiwa kuwa rais aliyepo madarakani ameonyesha dhamira ya kweli ya kuimarisha mifumo hiyo.
Raia Mwema