Utandawazi umeleta illusion of control

Utandawazi umeleta illusion of control

Gunner11

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2021
Posts
14,053
Reaction score
27,294
Unajua leo nilikuwa nawaza sana hapa, how utandawazi umeleta ujinga sana duniani badala ya maendeleo halisi.

Ni kwamba siku hizi mtu anaweza akaamka asubuhi akaanza kuongelea watu vibaya, na wengine vizuri na hiyo ndo ikawa career yake.

Mtu anaweza kuanzisha cult ya kuigiza anaumwa mtandaoni au akatumia mgonjwa kupata pesa. Wakati akimpatia hela kidogo na yeye kuchukua asilimia kubwa.

Mitandao imebadilisha taswira ya mahusiano, siku hizi watu wanapendana kwa picha za mitandao, mtu ana swipe page ya Instagram anachukua mzigo. No wonder why ndoa hazidumu. Maana hauwezi kujua mtu kwa kuswpie picha zenye highlight reels.

Yaani utandawazi umebadili kabisa namna bora ya kuishi, tumekuwa mazombie tunaotembea. Dhana ya kitu kizuri na bora imebadilika kabisa, maudhui yatokayo mitandaoni na uhalisia wa vitu vya nje ni tofauti kabisa.

Watu wanaona fahari kuishi maisha ya kuigiza mitandaoni wakati ukweli ni kwamba hata milo yao ya siku ni ya kubangaiza.

Binafsi huwa naomba siku itokee internet imepotea ghafla na kila kitu kirudi miaka ya 90 huko, watu wawe na elimu walivyo itesekea darasani, wawe na ujuzi timamu na Hakika walioupata kupitia miaka nenda rudi ya kujifunza. Kuwa na Mahusiano yenye nyama kubwa sio kalio na lips denda tu. Kuwe na wanawake wanaojuwa real struggle ya mwanaume sio hawa wanakesha bar wakisubiri maokoto. Kuwe na kupeleka posa na kujumuisha wazee kabla ya kuoa au kuolewa.

Napenda sana mambo ya rudi nyuma japo kuwa tumekuwa kipindi mambo ndo anaanza kubadilika.

Ila hata kama hayatabadilika ni jukumu la kila mtu anaye taka kurudi nyuma kuanza sasa Kuya design maisha yake kila siku Kadri anavyoweza kuweka muda wa ku incorporate namna ya kuishi inayo wiana na maisha hayo, yaweza kuwa kusoma vitabu vya enzi hizo, kuonana na Wazee, kumchukua mchumba wako na kwenda nje ya mji kuinjoi peke yenu, ni namna nzuri itakayo kufanya kuanza kuadapt mdogo mdogo kwenye hii reality inayo zidi kupotezwa na AI namaisha ya kuigiza mtandaoni.

Real life ni sasa wakati huu..

Buddha alisha wahi kusema

Before Enlightenment chop wood fetch water, after Enlightenment chop wood fetch water
 
Inategemeana na jinsi unavyoitumia, huwezi kusema magari ni mabaya kisa yanaua watu kwa ajali.... wakati watumiaji ndio wanazingua...

Internet sio kiumbe hai na haielewi wala haisikii chochote!
 
Inategemeana na jinsi unavyoitumia, huwezi kusema magari ni mabaya kisa yanaua watu kwa ajali.... wakati watumiaji ndio wanazingua...
Kumbuka utandawazi na technolojia ni vitu viwili tofauti unaweza kukaa na technolojia ila utandawazi ukawa wa kawaida nikiwa na maana mtu akatumia technology kudumisha kile kilicho na manufaa..
Internet sio kiumbe hai na haielewi wala haisikii chochote!
Ni kweli na katika maandiko yangu sijagusia internet yenyewe nimegusia namna matumizi yake yamekuwa mabaya
 
Kumbuka utandawazi na technolojia ni vitu viwili tofauti unaweza kukaa na technolojia ila utandawazi ukawa wa kawaida nikiwa na maana mtu akatumia technology kudumisha kile kilicho na manufaa..

Ni kweli na katika maandiko yangu sijagusia internet yenyewe nimegusia namna matumizi yake yamekuwa mabaya
Ni kweli umesema "itokee hata siku moja internet ipotee" ....inategemeana kama inaleta hasara kubwa sana kuliko faida na hakuna njia za kuidhibiti ni bora ipotee tu mkuu..
 
Kuna mambo yanaishia kwenye mawazo au nadharia tu.

Hakuna namna uta reverse hayo mambo labda uamue kuishi maporini na wasandawe.
 
Kwa leo mleta mada, umechukia sana mtandao, sijui umekutana na nini huko, mana umeitamani ile block down ya Mo29 jinsi walivyozima switch wiki nzima. Lisu na submission yake ametrend kisana tu. Nchi yetu sote sio ya walamba asali peke yao wanaohofia mitandao
 
Kuna mambo yanaishia kwenye mawazo au nadharia tu.

Hakuna namna uta reverse hayo mambo labda uamue kuishi maporini na wasandawe.
na huko porini ni ngumu kuishi maisha ya ukale, labda uwe umezaliwa hukohuko porini na hujui dunia nyingine
 
Au urudi kijijini ndani ndani kabisa... halafu ukutwe na el nino hata hujui na haujafanya maandalizi yoyote ndio utajua hujui..
el nino ndiyo kitu gani wewe? Mvua zipo miaka na miaka, chache na nyingi, ni kawaida mvua kunyesha katika msimu wake
 
Back
Top Bottom