Utamu au uchungu ..!?

it depends on how one was raised up the morals and the like

Kuna kinachostahili hongera kikakosa basis?

If there is basis kwanini zisiaply kwa wengine?
 
wala besti usifungue hiyo thredi kwani utajaza server bure hapa panapotosha kukupa ushauri

wewe umefanya jambo la mbolea kama kweli hujamgusa huyo mbinti wa watu, endelea na msimamo wako huohuo wala usiache ila msigusane mtawaka tamaa na kufanya hicho kitendo lala
cha kufanya wewe kaa na huyo binti mweleze kuwa hutaki kufanya KITENDO LALA mpaka ndoa yenu ifike
na ndoa ikifika niite mm niwe MSHENGA wa hiyo ndoa yenu

 
thamani ya ndoa ni ile hali ya watu wawili waliomo kwenye mapendo
pasipo kushirikiana kabla na kushirikiana baada ya KITENDO LALA

hiyo ndo thamani ya ndoa kwani mshiriki kwenye KITENDO LALA mapema
kunaleta kutokuaminiana tena kwani uaminifu huondoka kwa kuwa pamoja
kabla pasipo baada ya ndoa

Thamani ya ndoa ni mambo mangapi?
 

Kwahiyo kwa maelezo yako haya thamani ya ndoa ni Tendo la ndoa,si ndio?
 
Hata brand NEW CAR kabla haijaingia sokoni TEST is a MUST
But kwa wabuduo/wakristo ni DHAMBI kuonja kabla ya kuhalalishwa!
:israel:
 
Kumbuka serekalini ukiishi na mtu kwa muda wa miezi 6 kwenye chumba kimoja na mkawa na uhusiano, tayari ni mkeo

so iwapo wameishi pamoja hiyo miezi sita au zaidi na ikitokea mwanaume anataka kuoa, mwanamke anaweza zuia hiyo ndoa au?
 

dah! sisi enzi zetu ndoa ilikuwa zaidi ya kujamiiana. ndoa ilikuwa ni sawa na kuongeza ukoo, hivyo ilituwia rahisi zaidi kuoa kijijini tutokako kwani tulikuwa tunaoa katika ukoo tunao ufahamu vyema. hata kama akitokea mtu kuoa nje ya kijijini kwake basi ilikuwa shurti kupeleleza huo ukoo au watu wachache watokao ukoo huo.

siku hizi naona vijana wetu wanalenga kwa binti. kumfahamu binti ndio kigezo tena sio kumfahamu tabia tu, bali pia katika yale mambo. ndio hapo unakuta mtu anataka kuishi kwanza na binti kwa kisingizio cha kufahaminiana. bahati mbaya siku hizi usanii ni mwingi hivyo watu huficha "makucha" katika hicho kipindi cha kufahaminiana. na makucha hayo hutokeza iwapo ndoa itatokea. hii ukichanganya na ndugu unaoanza kuwafahamu baada za ndoa basi hukawii kusikia watu wakilalama "ooh mi sikujua...ooh, mawifi hivi, mama mkwe vile, shemeji nae!...".

kuishi pamoja kabla ya ndoa haisaidii ndoa ni fix tu...
 
Mie kwa maoni yangu kuishi pamoja kabla hamjafunga pingu za maisha si sawa maana mara nyingi hasa wanaume baada ya hili kutokea wengi wao huanza kusogeza kalenda kuhusu ni lini harusi itafungwa na hatimaye miaka hukatika hata anayetaka kuolewa kukata tamaa na kuacha kuulizia. Kuhusu tendo la ndoa pamoja na kuwa vitabu vya dini haviruhusu hili kabla ya ndoa dunia ya leo imebadilika sana watu wanajua mengi sana kuhusu tendo la ndoa. Hivyo kabla ya kufunga pingu za maisha wengi hupenda kujua kama kuna compatibility kwenye idara hiyo au ni midebwedo tu. Wahusika wakisharidhishana katika idara hiyo basi pingamizi linakuwa halipo tena.



 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…