Inawezekana akafika mwisho wa term yake hapo 2030
Je kuna yapi ambayo wewe unadhani atakumbukwa kwayo.
Yawe mabaya au mazuri
Uwanja ni wako
My friends ladies and gentlemen,
Kwanza kabisa,
taifa litamkumbuka Rais Dr.Samia Suluhu Hassan kwa ujasiri, uthubutu na umadhubuti wake wa kukubali kuipokea nchi katika mazingira magumu, kuidhibiti, kuipitisha na kuiongoza katika kipindi kigumu cha majonzi na hatari zaidi za usalama kufuatia kifo cha aliekua Rais wakati huo hayati DR JPM. Hapa, Dr Samia Suluhu Hassan alionyesha umahiri wa kiwango cha juu mno katika uongozi wa taifa.
Lakini pia,
hatua ya Rais Dr.Samia Suluhu Hassan mara tu baada ya kushika hatamu za uongozi wa nchi na kuamua kwa makusudi kabisa, kuifungua nchi miongoni mwa mataifa ya ulimwengu, na kuliunganisha taifa kwa falsafa ya 4Rs, hakuna mTanzania anaweza kusahau jambo zito na la maana zaidi kama hili.
Zaidi sana,
falsafa za Dr Samia Suluhu Hassan kama "Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, kazi iendelee" au "kazi na utu tunasonga mbele pamoja "ni mambo yatakayoishi milele yote miongoni mwa vizazi vya waTanzania.
Rais Dr.Samia Suluhu Hassan kukamilisha kwa kishindo miradi mikubwa ya kisasa na yakimkakati kama vile treni ya SGR, bwawa la umeme la mwalimu Nyerere, ujenzi wa zahanati kila kijiji, kukomesha kabisa tatizo la umeme, kuimarika kwa hali ya usalama nchini na kuongeza uwekezaji nchini ni miongoni mwa mambo machache sana kati ya mengine mengi sana yatayokafanya waTanzania kutomsahau Rais Dr Samia Suluhu Hassan maisha yao yote 🐒