Utambulisho mpya wa Jiji la Dar es Salaam

Utambulisho mpya wa Jiji la Dar es Salaam

Jiji la Dar es Salaam linakuwa kwa kasi kubwa,
Miaka ya zamani jiji hili lilikuwa linatambulishwa kwa kuona picha ya ghorofa la kitega uchumi (ukiachilia mbali mnara wa askari), baadae yakajengwa majengo mengine marefu na jengo la kitega uchumi likafunikwa, likaja jengo la Benjamin Mkapa Tower, (Zamani mafuta house), na sasa zama za jengo la benjamin mkapa tower pamoja na PPF tower zimeshapita, na kwa sasa utambulisho mpya ni haya majengo yaliyopo jirani, ghorofa la PSPF pamoja na ghorofa la One Bandari tower ambayo yote yapo Sokoine drive.

Hii ni tofauti na jiji la Nairobi ambalo miaka nenda miaka rudi limekuwa likitambulishwa kwa picha za jengo la kituo cha mikutano cha Kenyatta.

View attachment 254261
Bado kabisa kunahitaji mabadiliko makubwa katika Jiji letu Miundo mbinu bado mibovu hakuna barabara za kisasa mifereji ya maji sio mizuri Mvua ikinyesha Mjini Dar kunageuka kuwa ni bahari au ziwa bado kabisa Mkuu wa mkoa wa halmashauri kuu ya mkoa na Mkuu Meya wa jiji la Dar sijuwi wanafanya kazi gani?
 
Uzuri wabongo tunajijuwa sifa zetu. kwenye mafanikio yetu ndio huwa hatupendi, tukiludi kwenye ukweli majengo hayo ni mazuri pia ni kivutio cha jiji la dar es salaam. bila kujali jiji limepangwaje, na ndio majengo marefu ukanda wa afrika mashariki, kati,mpaka magharibu kwa kipindi hichi, mnatake msitake, lakini bado mnakandia, hata hilo jiji la nairobi mnalolisifia tofauti ni ndogo sana. nairobi inautajiri wa barabara na nafasi, ila kimajengo sawasawa tu dar es salaam
 
upo sahihi, tatizo watz walio wengi tumezoea kulaumu kila kitu, hawatak kukubali ukweli.
 
Dar bado sana kuingia katika ligi miji mizuri iliyopangwa vizuri kama Nairobi.Hata ukiangalia hiyo picha ni majengo duni yaliyojengwa katika nafasi finyu yenye mandhari isiyovutia.Haiewzekani kuibadilisha Dar kuwa mji wa kisasa,Huu mji unafaa kubakia kama mji mkongwe na badala yake kujenga mji wa kisasa nje kabisa ya jiji hili.
kweli kabisa unayosema.
 
Mkuu asante kwa taarifa but usingejaribu kulinganisha Dar na Nairobi kwa sababu kwa majengo mazuri na ya kisasa Dar hayawezi kulinganishwa na Nairobi hata kidogo.

dar es salaam uifananishe na mombasa lakini sio NAIROBI

Yani dar unailinganisha na nairobi hata bila aibu?dar size yake ni akina bujumbura,kampala,kigali na kinshasa.

Dar bado sana kuingia katika ligi miji mizuri iliyopangwa vizuri kama Nairobi.Hata ukiangalia hiyo picha ni majengo duni yaliyojengwa katika nafasi finyu yenye mandhari isiyovutia.Haiewzekani kuibadilisha Dar kuwa mji wa kisasa,Huu mji unafaa kubakia kama mji mkongwe na badala yake kujenga mji wa kisasa nje kabisa ya jiji hili.

Hizi ndio kauli za watu ambao upeo wao umeishia Nairobi
 
utofauti uliopo kati ya dar na nairobi kiukweli ni mdogo mno.....na kila nikitazama kati ya miji hii ni upi baada ya miaka kumi utakua mkubwa zaidi kuliko mwingine kiukweli Dar es salaam unaonekana kukua zaidi
 
Mji si lazima uwakilishwe na alama ya jengo refu au la kisasa kupita yote kwa kuwa technologia ya ujenzi inabadilika klia siku. Inatakiwa alama maalumu ya kihistoria au vinginevyo. Rio de Janeiro - sanamu ya yesu, Paris - mnara wa Eiffel, New York - liberty statue, Arusha - clock tower, Monduli - ...

Alkaaba =Maka Saudi Arabia
 
Back
Top Bottom