2013
JF-Expert Member
- Aug 2, 2011
- 11,365
- 6,086
Katika fuatilia fuatilia yangu ya hali za kisiasa nchi mbalimbali duniani, nimegundua kwamba nchi zenye asili ama jamii za waarabu hazitawaliki kwa kufuata neno hili la demokrasia. Pengine hazitaki demokrasia kwakuwa sio utamaduni wao kama ilivyozoeleka kuwa demokrasia asili yake ni nchi za magharibi. Ili Amani iendelee kuwepo nchi hizi zinahitaji kiongozi dikteta ama mungu mtu , mwinyi, mfalme atakaye amua mustakabali wa jamii nzima. Nchi hizi kuruhusu demokrasia inakuwa ni sawa na kuruhusu vurugu na mauaji. Hata kama ni kwa nia njema ama vyovyote vile, wananchi wake hawana furaha na wako tayari kufa kwa style yoyote ile yaani hawana cha kupoteza pengine wana upeo finyu ama hisia kali ama vyovyote vile lakini vurugu na mauaji hayataepukika. Hata pale penye uwelekeo wa demokrasia wananchi wanaonyesha viashiria vya uvunjifu wa Amani kwa namna mbalimbali huku wakibariki kuwa ni sehemu ya demokrasia pia(mfano maandamano ya vurugu) na huku wakidai hakuna haki. Nchi hizi zinapiga hatua ya maendeleo ikiwa tu zinatawaliwa na viongozi wasioachia madaraka (kama wafalme ama madikteta na wanajeshi)---. Nchi hizi zinaongoza kwakuwa na sheria kali zinazobaka uhuru wa watu kuishi kwa furaha, ambapo sheria hizi zinatekelezwa kwa adhabu kali sana ikiwemo adhabu kuu ya kifo cha kikatili sana. Viwango vya haki kuhusiana na adhabu hizi pia ni un-questionable na mara nyingi zipo kinyume na sheria za haki za binadamu duniani. Viongozi/madikteta/wafalme/mamwinyi wa nchi hizi wanapofanikiwa kutawala bila vurugu ndio kiashiria pekee cha haki na kuridhika kwa wananchi kuhusiana na mambo yanavyoendeshwa katika siasa za kimataifa. Japokuwa uhalisia haupo hivyo. Mifano michache yakuliona hili ni kama Egypt wakati na baada ya mubarak, Libya wakati na baada ya gadafi, Iraqi wakati na baada ya sadam, Nchi nyingine ni Afghanistan, Somalia, Pakistan, Iran, Syria, Somalia, Saudi Arabia, northern Sudan, just to mention a few. kimsingi nikitolea mifano nchi za misri na libya hazikuwa na uhuru wala haki lakini zilifanikiwa sana kama nchi zenye neema, na pale demokrasia ilipoingizwa ndipo haki inapoonekana haitendeki, ili amani iwepo inahitajika udikteta tu, kwani wananchi hawahofii kuuana kama somalia. the fittest survive. Ni mtazamo tu wana jf naomba maoni yenu…..