Utakubali kwenda kupima DNA endapo itatolewa bure?

Utakubali kwenda kupima DNA endapo itatolewa bure?

STUNTER

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Posts
13,077
Reaction score
17,260
Kwenye kizazi cha sasa hofu inazidi kutanda kwa wazazi hasa wa kiume
juu ya umiliki halali wa watoto.

Na hii yote imetokana na wapenzi kukosa uaminifu na kutokuwa wakweli,
Mungu si Lipumba kikavumbuliwa hiki kipimo cha DNA lakini kinyume na matarijio, wanawake wengi wameonyesha kukichukia kupita kiasi,

Anyway hebu tuambie endapo utapewa ofa ya kwenda kupima DNA, ikijumuisha kipimo cha wazazi wako ili kujua kama ni wazazi wako halali
Vilevile kipimo cha mtoto/watoto wako,
UTAKUBALI KWENDA KUPIMA?
(unaweza kusema kipimo kipi utakikubali kwenda kupima na kwanini)
 
Mimi kiroho safi nakubali kwenda kupima kwa maana najiamini
 
Swala la kwenda kupina inawezekana ila utata unakuja kwenye upokeaji wa majibu kuna hasi na chanya kwaiyo si jambo la kushangqza
 
Hebu mtu mmoja ajitokeze hapa kwamba alienda kupima DNA( TZ) kisha akapewa JIBU huyu sio MTOTO wako.... always Jibu huwa unapewa huyu Wako.

Zimwi likujualo......
 
Mimi nimefanana na baba yangu. Na ndugu zangu upande wa baba hata kama wananiona leo wananiuliza wewe ni mtoto wa mzee fulani? Nawajibu haswaa ndiye mimi umejuaje? Anajibu sura tu inaonyesha.

Basi najiamini kwamba kuzaliwa kwangu hakukua na goli la mkono.
Ikitokea DNA itakuwa ni sawa tu kupima au kutopima no effect.

Japo sina mtoto bado.
 
Kuna watu wanafanana na baba zao kweli kweli sidhani kama wana haja ya hiyo kitu
 
Matokeo yanaleta hofu, ukimwambia mke tupime kama mtoto ni halali yako huwa anasita. Yeye anajua ni wake kwani kamzaa anahofia nini kama anajiamini? Mashaka yananiletea wasiwasi. Huenda siku ya mimba alichepuka hivyo wasiwasi. Mkubali jibu lolote litapokelewa kumbuka kitanda hakizai haramu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swala la kwenda kupina inawezekana ila utata unakuja kwenye upokeaji wa majibu kuna hasi na chanya kwaiyo si jambo la kushangqza
Kwahiyo wewe ungepima au usingepima?
 
Hebu mtu mmoja ajitokeze hapa kwamba alienda kupima DNA( TZ) kisha akapewa JIBU huyu sio MTOTO wako.... always Jibu huwa unapewa huyu Wako.

Zimwi likujualo......
Whats the secret behind of curtain?
Kumbe ndiyo hali halisi?
 
Back
Top Bottom