The Boss
JF-Expert Member
- Aug 18, 2009
- 49,320
- 117,672
Nitakwambia siku
Ntasubiri
Nitakwambia siku
Na mimi nilitaka kuuliza swali hiloNitakwambia siku
Mifano mizuri sanaKwa mfano unauza ng'anda ukipata ile hela unaweza kwenda kukopa bank ukawa unarudisha kidogo kidogo wakati huo unanunua au kujenga majumba unanunua labda magari ya usafirishaji wengine wafungua microfinance ndo utakatishaji sasa watu wanakuona uko busy na mabiashara kumbe hayo mabiashara hayana faida za kihivyo
ni tu kama Jamali Malinzi yeye alipewa hela za kujenga uwanja mkubwa wa mpira akaenda kukarabati eneo la CCM pale kaitaba.
kuosha fedha kwa sabuni ya unga na brush hadi zitakate na kurudi kwenye hali yakeUnajua huwa sielewi maana ya utakatishaji wa fedha wajuzi mnijuze maana hapa huwa sielewi kabisa
Kumbe ndo hivyo eehexactly, sawa na mtu anafanya wizi wa karne,anazama bank halaf anaiba trillion nzima,sasa ili usishtukiwe kwa kumiliki hicho kiasi ilihali huna chanzo cha kipato kinachokidhi ndo anaamua kuanzisha labda kampuni la kamari,au anakopa bank ili aanzishe biashara na anakuja kuripa mkopo kwa ile ile hela alopiga,then anakuja kumiliki ma business ambayo hata bank accounts zake zikisoma anatriolion nzima hakuna atakayebisha,huyo atakuwa katakatisha,over
ShukranKutakatisha fedha ni pale ambapo umepata pesa kinyume na utaratibu ambao ni halali, mfano umeuza madawa ya kulevya, umekwambua pesa escrow, umeajiriwa kama TRA, TPA, TBA kisha ukaiba pesa. Katika mazingira kama hayo, chukulia mfano umeiba 300,000,000.
Kutakatisha fedha kuna hivi, unachukua hii pesa unaenda kununua mfano toyota coaster ya 45,000,000 ili kila siku ikuletee hesabu. Unaponunua hii gari kumbuka umelipa gharama za bandari, TRA, leseni n.k ambavyo vyote ni halali kisheria. Kwahiyo pesa ambayo wewe utaipokea ni halali kabisa hauwezi ukafungwa na sheria yoyote.
Mfano wa pili, umeenda kununua kiwanja, utapewa hati miliki zote za kiwanja wakati pesa ambayo wewe uliyoitumia kupata kiwanja hukuipata kihalali ila unamiliki mali ambayo ni halali kwako.
Ni kitendo cha kuifanya pesa ambayo sio halali sehemu flani na kuifanya iwe ni halali sehemu flani.
fanya tu practical nenda kafanye ujambazi au biashara yeyote illegal alafu uje ufungue duka ni ngumu sana kukamatwaUnajua huwa sielewi maana ya utakatishaji wa fedha wajuzi mnijuze maana hapa huwa sielewi kabisa
kutakatisha=kutakasa ,,,,,,yaani hela iliyopatikana kwa njia haramu unaiingiza kwny mzunguko wa fedha halali,,,,,,yaani kuihalalisha fedha haramu,mfano umeuza ngada ukafanikiwa kupush bila kudakwa,sasa ukaanza maneuver ya kuiweka hela hiyo kwny mzunguko wa fedha ili ianze kutumika dingi,hapo ndo utakuwa unatakatisha,,,,,,kwa uelewa wangu mfinyu najua hivyo