Utakapokuwa Umejenga Nyumba yako usisahau hili

SuperImpressor

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
1,504
646
Biblia nayo haikubaki nyuma kutoa ushauri kwa wanaotaka kujenga nyumba mpya.

Kumbukumbu la Torati 22:8
[8]Utakapojenga nyumba mpya, fanya ukuta kando-kando ya dari lako, usije ukaleta damu juu ya nyumba yako, mtu akianguka huko.

Sent from my cupboard using mug
 
Weka picha ya ukuta kando kando ya dari
Mfano hayo majengo yote unaona kila floor dari yake ina kauzio kwa nje ingawa hilo jengo jingine vizio vyake viliwekewa vyuma badala ya ukuta.

Kwa hiyo dari ya kila floor imeungana na uzio(ukuta) wake kwa nje

Biblia kitu kingine bwana. Maghorofa yalianza zamani sana
Screenshot_20210730-115404.jpg



Sent from my cupboard using mug
 
Ndani ya bible, dari ni nyumba

So anaposema ukuta kando kando ya Dari yako anamaanisha, ukuta kuzunguka nyumba yako.

Niko tayari kurekebishwa.
Ni sawa, lakini ukuta wa nyumba unazuiaje mtu asimwage damu kwa kuanguka? Au ulikuwa hujasoma vizuri?


Sent from my cupboard using mug
 
Tutaweza kuelewa andiko baada ya kupitia maandiko

Hebu kwenye hiyo aya (mstari) anzia nyuma kidogo kisha nenda mbele kidogo
 
Huko kuanguka, Bible haikumaanisha kuanguka kutoka juu ya kitu

Mtu anaweza akaanguka tu hapo kutokana na sababu mbalimbali.
Pole sana ndugu yangu, dari siyo nyumba ila ni sehemu mojawapo iliyo kwenye nyumba unamokaa wewe.


“Hata walipokosa nafasi ya kumpeleka ndani kwa ajili ya lile kundi la watu, walipanda juu ya dari wakampisha katika matofali ya juu, wakamshusha yeye na kitanda chake katikati mbele ya Yesu.”
— Luka 5:19 (Biblia Takatifu)

“Katika siku ile, aliye juu ya dari, na vyombo vyake vimo ndani ya nyumba, asishuke ili kuvitwaa; na kadhalika, aliye shambani asirejee nyuma.”
— Luka 17:31 (Biblia Takatifu)


Sent from my cupboard using mug
 
Nadhani kilichomchanganya ni hiki;


“Yule akida akamjibu, akasema, Bwana, mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu; lakini sema neno tu, na mtumishi wangu atapona.”
— Mathayo 8:8 (Biblia Takatifu)

“Ni afadhali kukaa katika pembe ya darini, Kuliko katika nyumba pana pamoja na mwanamke mgomvi.”
— Mithali 21:9 (Biblia Takatifu)


Sent from my cupboard using mug
 
Hili fungu linanithibitishia kwamba dari......

“Ikawa wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani, akatembea juu ya dari ya jumba la mfalme; na alipokuwa juu ya dari aliona mwanamke anaoga; naye huyo mwanamke alikuwa mzuri sana, wa kupendeza macho.”
— 2 Samweli 11:2 (Biblia Takatifu)

"Dari" ni noma kweli aisee


Sent from my cupboard using mug
 
Hili fungu linanithibitishia kwamba dari......

“Ikawa wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani, akatembea juu ya dari ya jumba la mfalme; na alipokuwa juu ya dari aliona mwanamke anaoga; naye huyo mwanamke alikuwa mzuri sana, wa kupendeza macho.”
— 2 Samweli 11:2 (Biblia Takatifu)

"Dari" ni noma kweli aisee


Sent from my cupboard using mug
Huo mjengo ulikuwa ghorofa sio kitoto
 
Huko kuanguka, Bible haikumaanisha kuanguka kutoka juu ya kitu

Mtu anaweza akaanguka tu hapo kutokana na sababu mbalimbali.
“Kijana mmoja, jina lake Eutiko, alikuwa ameketi dirishani, akalemewa na usingizi sana; hata Paulo alipoendelea sana kuhubiri, akazidiwa na usingizi wake akaanguka toka orofa ya tatu; akainuliwa amekwisha kufa.”
— Matendo ya Mitume 20:9 (Biblia Takatifu)

Ule ukuta ungekuwepo kwenye hilo jengo huyo kijana asingekufa.


Sent from my cupboard using mug
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom