Mwanadamu ameumbwa na tamaa, nikimaanisha kuwa na mataminio katika mapenzi, hivyo kupenda inachukua muda mchache na ni nadra sana kukuta wapenzi wawili kupendana kwa dhati kwa muda mrefu hata mpaka mwisho wa maisha yao.
Na ikumbukwe kuwa hakuna mwanadamu aliyekamilika ni lazima atakuwa na kasoro katika jambo Fulani.
Mfano: utakuta mwanaume & mwanamke anampenda mpenzi wake kwa kumjali, kumfanya awe na furaha muda wote, kuhakikisha analinda penzi lake, anamtosheleza kimapenzi, lakini ni kwa muda tu na baada ya hapo anatafuta mpenzi mwingine,
Lakini kwa hii kizazi cha sasa mambo yamebadilika kwa kiasi kikubwa mno hususani katika suala la mapenzi, mapenzi ya sasa yametawaliwa na pesa.
Kwa hiyo itabidi uishi kulingana na mazingira
Kwa sasa ni ngumu kupata ama kujua kuwa ni yupi mwenye mapenzi ya dhati. Ingawa sio wote ambao hawana mapenzi ya dhati ila asilimia kubwa mapenzi yametawaliwa na pesa, tamaa, uongo,
na tusikariri kuwa hamna mapenzi ya dhati yapo ila ni kwa asilimia ndogo sana. Hivyo unahitajika kuishi kutokana na mazingira husika kwa sababu hata mifumo na baadhi ya mambo hubadilika.......