Utajuaje unapendwa toka rohoni?

Utajuaje unapendwa toka rohoni?

ZEE LA HEKIMA

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2015
Posts
1,422
Reaction score
1,851
Wana JF hebu changieni kila mtu aeleze anajuaje kwamba mpenzi wake anampenda kweli toka rohoni?

Nasubiri michango yenu.
 
Nikiona simuombi hela, na yeye hajisifii hela

Hapo moyo kuntu!
 
Mmmh! Hapa pagumu! Kwenye ishu ya mapenzi ufeki mwingi saana na inawezekana mtu ukazeeka na bado hujawai penda.
Nnavyodhani, Mapenzi ya kweli ni pale unapojua mazuri na mabaya ya mtu na bado unamjali na kumthamini. Ata ukigundua msichana ni mwizi utazidi kumweka karibu na kujaribu kumbadilisha.
Mimi siamini kama mapenzi yanakuwepo kabla hamjafahamiana vizuri.
Tunachofanya wengi wetu ni maigizo tu!
 
Atakuheshimu
Atakuthamini
Tatizo lako lake
Atakwambia anakupenda
Haoni aibu kukutambulisha kwa yoyote
Hakuna siri kati yenu
Atakurekebisha ukikosea mkiwa ndani (sio mbele za watu)
Atatunza siri zako (sio mambo yenu anaropoka kwa watu)
Atafanya mapenzi na wewe tu(achepuki wala hana mawazo ya kuchepuka)
Atakua na malengo na wewe
 
Moyo wa mtu ni kiza kinene... hakuna jibu sahihi kwamba utajuaje... lakin matendo huwa yanaongea zaid kuliko fikra. So just angalia matendo ya mtu ulienae kwenye mahusiano... hata kama ana pretend.. kuna kitu utagundua.
 
Atakuheshimu
Atakuthamini
Tatizo lako lake
Atakwambia anakupenda
Haoni aibu kukutambulisha kwa yoyote
Hakuna siri kati yenu
Atakurekebisha ukikosea mkiwa ndani (sio mbele za watu)
Atatunza siri zako (sio mambo yenu anaropoka kwa watu)
Atafanya mapenzi na wewe tu(achepuki wala hana mawazo ya kuchepuka)
Atakua na malengo na wewe
Wachache sana wanaotimiza yote haya...
 
Atakuheshimu
Atakuthamini
Tatizo lako lake
Atakwambia anakupenda
Haoni aibu kukutambulisha kwa yoyote
Hakuna siri kati yenu
Atakurekebisha ukikosea mkiwa ndani (sio mbele za watu)
Atatunza siri zako (sio mambo yenu anaropoka kwa watu)
Atafanya mapenzi na wewe tu(achepuki wala hana mawazo ya kuchepuka)
Atakua na malengo na wewe

Hapo uliposema atakua achepuki..kwa kigezo hicho mhhhh [emoji57] [emoji57] [emoji57]
 
Nendeni hospital alaf mpime kipimo kinaitwa ultra sound majibu cku hyo hyo
 
Love is easily demostrated than spoken. Halafu kwqngu naona mioyo kama inaongea. Kama unampenda mtu na kma na yeye anakupenda mioyo inazungumza
Tokea uache ile tabia mbaya ya nzi umekuwa na akili.
 
Yaani mimi nisipokuomba hela ujue hata kwenye kidole haupo, huo upande mwingine siwezi usemea moyo.
 
Atakuheshimu
Atakuthamini
Tatizo lako lake
Atakwambia anakupenda
Haoni aibu kukutambulisha kwa yoyote
Hakuna siri kati yenu
Atakurekebisha ukikosea mkiwa ndani (sio mbele za watu)
Atatunza siri zako (sio mambo yenu anaropoka kwa watu)
Atafanya mapenzi na wewe tu(achepuki wala hana mawazo ya kuchepuka)
Atakua na malengo na wewe

Tatizo haya hayadumu ndio shida, bora mpelekane kimafia tu. Utamfanyia yote hayo mtu still atakuumiza.
 
Kwani mambo ya kupendana kutoka moyoni bado yapo??
 
Back
Top Bottom