Utajuaje kama una laana ?

Utajuaje kama una laana ?

Samia atosha tukutane2030

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
17,190
Reaction score
48,705
Laana ni nini?
Kwa mujibu wa Biblia laana ina maana kadhaa wa kadhaa ikiwa ni pamoja na;

1. Kuwa na maisha yasiyo zaa

2.Kutambaa (kuwa na hatua hafifu kwenye maisha)

3.Kufa, hapa namaanisha kifo cha mwili au kuishi maisha kama mfu. Au kuishi mahali ambapo kila kitu kimekufa.

4.Kuzaa watoto wasio na tija kwa jamii au kwako.
N.k, n.kDalili za laana.

Kabla sijakupa dalili za laana ni vyema pia kitambua kuwa laana inaweza kuwa sehemu husika tu. Mfano: Wewe mwenyewe unaweza kuwa huna laana lakini kazi yako ina laana.

Laana inaweza kuangukia kwenye nyumba, kazi, shamba, watoto n.k
Laana inaweza kukupata toka kwa Mungu mwenyewe, shetani, lakini shetani hana nafasi ya kukupa laana labda wewe mwenyewe uwe uliacha mlango wazi. yaani uliweka mlango halali, Legalized. Wewe ndiye unaweza kumpa mchawi, pepo na shetani akulaani pindi unapoacha njia za Mungu.
Dalili za laana
.
Kutokuwa na makazi ya kudumu.
Leo Arusha, kesho Moshi, keshokutwa Dar mara Singida.
.Kutokupata mapumziko.
Ukiona maishani mwako kila siku uko busy huna muda wa kuoumzika au kuenjoi na familia yako hiyo ni dalili ya laana.
.Kukataliwa .

Cheti chako kinaweza kuwa kiko na GPA ya juu lakini ukiwa na laana watu hawakipi uzito wanaona kama umeokota tu. Kila mahali unakataliwa.
.Kutokustawi.

Yaani shati la mwaka juzi mpaka leo unatamba nalo, mpaka boxer zako zinapauka.
.Njaa na ukosefu ndani ya nyumba yako.

Haijalushi umeajiriwa au kujiajiri , kila siku familia yako iko kwenye uhitaji mkubwa. Hiyo ni laana.
.Kutokuzaa au watoto kufa wakiwa wadogo, kabla hawajakomaa. Hapo kuna laana.

Namna ya kujitoa kwenye laana.
Jambo muhimu kabisa ni lazima ujue sababu ya hiyo laana. Kujua tu ni hatua tosha, hatua ya pili kuomba toba na kuifuta kwa jina la Yesu. sio damu ya Yesu ni jina la Yesu. Damu ya Yesu haifuti laana, damu ya Yesu inadeal na dhambi na wokovu tu.

Lazima tujue kuomba vizuri tusiishi kwa mapokeo tu.
Hatua nyingine ya kuondoka kwenye laana ni kuombewa na mtu mwenye baraka.
Laana ya kizazi ombewa na mtu mwenye baraka ya kizazi, laana kwenye uchumi ombewa na mtu aliyebarikiwa kwenye uchumi.
Kipofu akimuongoza kipofu matokeo yake mnayajua.
Hallelujah
 
Back
Top Bottom