Utajiri wa vijana wa Magufuli (RCs) una siri gani?

Utekelezaji wa matukio yale ndio chanzo kikubwa cha pesa kwa yule jamaa wa Dasilamu..
 
Matajiri wasasa sio wafanya biashara tens kwasasa ni wanasiasa, pesa yooote inavutwa serikalini alafu gemu inaanzia hapo unachotakiwa kama mwanasiasa ni
- act kama huna
- toa misaada mara kwa mara
- tumia maguvu kujidai unatetea wanyonge.
Alafu kesho nikapange mstari eti nachagua kiongozi??!! Bora nkapalilie magugu
 
Fanya kazi.... Ukiwa RCs una takiwa na 10,000 tu... Hii ndio roho mbaya aliyo isema Edo kumwembe...

Mtanzania kulipwa mshahara wa 8M, 18M 25M si sawa ila mzungu ktk nchi yako akilipwa dolls 50,000/- ni sawa...

Roho mbaya...! Na ingekuwa iyo timu ina tokea chato kunge kuwa hapatoshi mjini...

Ila mnyeti ni mkuu wa mkoa wa Manyara sio Mara
Jibu swali!! Ukwasi mkubwa kiasi hiki kwa mishahara ya RCs umetoka wapi?
Akili kama hizi zako kulipwa 8m ni matumizi mabaya ya pesa. Alafu unataka kulipwa sawa na mzungu!!! Unazani mzungu anaweza kujibu au kutoa hoja takataka kama hii!
 
Jibu swali!! Ukwasi mkubwa kiasi hiki kwa mishahara ya RCs umetoka wapi?
Akili kama hizi zako kulipwa 8m ni matumizi mabaya ya pesa. Alafu unataka kulipwa sawa na mzungu!!! Unazani mzungu anaweza kujibu au kutoa hoja takataka kama hii!
Una niuliza Mimi? Utajili una toka wapi? Una akili kweli?
 
Hizo pesa wanazipata kwa wafadhili...

Kinachotokea hao wafadhili hawapewi acknowledgment... badala yake wanajisema kama vile zimetolewa na wao wenyewe...


Cc: mahondaw
 
Ukiwa mfanyakazi wa umma huruusiwi kumiliki Mali wewe ni mshahara mpaka kifo?
Kwanza rekebisha uandishi wako huu Wa kingumbaro! Huruhusiwi na siyo huruusiwi!
Mali hukatazwi kuwa nazo kwani yawezekana nyingine ni za urithi na nyingine huenda Una vyanzo vinavyoeleweka na vilivyo wazi kwa kila mwenye kudodosa!
Hao kina Mnyeti na Makonda hawakuwa na background inayoonyesha kuwa na mali za urithi au zao wenyewe kwani kabla ya nafasi hizo za uteuzi walikuwa hawana source yoyote ya kipato ambacho unaweza kusema kimejiacummulate na kuuzaa ukwasi walionao kwa sasa! Makonda alikuwa uvccm na alikuwa akiishi kwa posho na zawadi na Mnyeti alikuwa mwalimu akiishi kwa kajimshahara kasikotosha kuishi kwa wiki mbili bila kukopa!
Itoshe tu kusema ukwasi wao unatia mashaka kwani hata wakuu wengine Wa mikoa waliowatangulia kuwepo hawana ukwasi walio nao! Mashaka haya yanatakiwa yawe na majibu ya kueleweka na kinyume chake utajiri wao Una ukakasi mkubwa! Haiwezekani uajiriwe kwa miaka minne nchi hii uwe billionaire hasa ukiwa unalipwa kwa scale zilizopo nchini!
Waje kivingine kujibu juu ya ukwasi wao na au wadeclare kuwa ni wafanyabiashara ya mihadarati au madini kwa kutumia nyadhifa zao! Na hii tume ya maadili mbona imelala Sana na au inaendekeza double standards?
 
Una niuliza Mimi? Utajili una toka wapi? Una akili kweli?
Dogo, Shule yako ni ya daraja gani? Utajili ndio nini? Halafu unahoji juu ya akili za wenzako! Super pathetic haiyumkini!
Mnajifanya kupambana na wauza ngada kumbe mnawapunguza ili kusababisha scarcity muuze ninyi! IPO siku mtaumbuka Kama hili la kugawa mabilioni mtaani kipapaa! Siku zenu zimefika ukingoni na huenda takukuru wanawachunguza bila ninyi kujua!
 
6Mil haiwezi kumpa miradi mingine? Je ulianza kumtambua akiwa RCs au kabla? Au shida ni baada ya kuwa RCs?
Andika kama mtanzania anayeishi Tanzania! 6m tshs kwa mwezi na kwa miaka mitatu huwezi kuwa billionaire hata Kama unaiweka bila kuitumia kwa miaka yote! Hata Kama utaiinvest haiwezi kukulipa hivyo! Tusijidanganye hapa kizumbukuku kwani wengine tumefanya biashara kwa muda mrefu na hatukuweza kumiliki mabilioni hata Kama tulikwepa kodi!
Kubali tu kuwa kuna utakatishaji au kupata mali through madaraka waliyonayo! Wachunguzwe!
 
Hii tabia ya wakuu wa mikoa kuomba fedha kwa wafanya biashara imepelekea kuepo kwa upendeleo ktk utoaji wa maamuzi.
 
Fanya kazi.... Ukiwa RCs una takiwa na 10,000 tu... Hii ndio roho mbaya aliyo isema Edo kumwembe...

Mtanzania kulipwa mshahara wa 8M, 18M 25M si sawa ila mzungu ktk nchi yako akilipwa dolls 50,000/- ni sawa...

Roho mbaya...! Na ingekuwa iyo timu ina tokea chato kunge kuwa hapatoshi mjini...

Ila mnyeti ni mkuu wa mkoa wa Manyara sio Mara
Naona umesahau kuwa jpm ndio roho ilimuuma watu kupata mishahara mikubwa akaishusha, je ana roho mbaya?
 
Back
Top Bottom