Glasnost
JF-Expert Member
- May 18, 2017
- 266
- 259
Kwa miaka mingi sasa Tanzania imekuwa ikijipambanua kimataifa kama nchi yenye vivutio vingi vya utalii na tamaduni mbalimbali. Hatua hii imesaidia kukuza utalii na hata kujenga uchumi imara na kutambulika kimataifa jambo lililofungua fursa kwa wawekezaji wa ndani kutumia nafasi hiyo kujipatia kipato na mafanikio kwa ujumla.
Lakini kwa mda mrefu sasa nchi hii imekuwa ikitumia mavazi na vitu vya kimasai kama utambulisho wa nchi ya Tanzania. Popote pale viongozi, wanamuziki na watu mashuhuri kutoka Tanzania wanapokuwa hasa ughaibuni hujitambulisha kwa utamaduni wa kimasai.
Kila mwanamitindo akiwa nje ya nchi katika mashindano ya urembo na mitindo, vazi la kuvaa ni la kimasai kama vile ni vazi la taifa au ndo njia pekee ya kuweza kujitangaza na imekuwa hivi mpaka leo. Ubunifu ni kitu kizuri na ndilo jambo la kufanya na sio mawazo mgando. Wamasai hata wakenya wanawatumia katika utalii na ubunifu. Sasa kama wakenya wanawatumia na sisi ni hivyo hivyo ni bora tukuze tamaduni za makabila mengine katika nyanja za kimataifa. Tanzania ni nchi kubwa na yenye utajiri wa mila,desturi na tamaduni za kuvutia mfano Wahehe na Wamakonde.
Inasikitisha na kuchekesha mda mwingine kuona hata waandishi,watangazaji katika makala na vipindi vyao kutilia msisitizo kwa Wamasai zaidi kana kwamba bila utambulisho wa kabila la Wamasai labda mtu wa nje anaweza hasiitambue Tanzania au hasieleweke. Ni jambo ambalo na uhakika kwa asilimia kubwa tu wengi mtashangaa inakuaje napinga utamaduni wa kabila fulani kupewa kipaumbele katika kulitangaza taifa la Tanzania.
Nachojaribu kuweka sawa hapa ni kwamba tuna makabila mengi tu hapa Tanzania hivyo basi tuonyeshe ukomavu wa kifikra na upeo kwamba Tanzania ni zaidi ya Wamasai na kuna tamaduni za kuvutia kutoka kwa makabila mengine.
Ni wakati sahihi sasa kwa wadau wa utalii, serikali na watanzania kubadilika na kubuni mbinu mpya za kukuza utalii. Mtu akiwa nje ya nchi awe kifua mbele kuvaa kinyamwezi, kimatumbi, kigogo na kujivunia utajiri wa tamaduni zetu. Najua kuna watu waoga na hawajiamini bila kuvaa kimasai itakuwa ngumu kutambulika unatoka wapi. Kwa watu kama hao, wakati umefika sasa kutojali utaonekana vipi. Hakuna mtu wa nje atakuja kukuza tamaduni zetu kimataifa bali ni sisi wenyewe.