Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amosi Makalla, akionyeshwa mgodi ujao wa Niobium
Madini ya Niobium ndio habari ya mjini. Badala ya STAMICO kuongoza tour ya kuionyesha serikali huyu mchimba madini mpango wake ni vipi, unakuta anaekuja kuchimba vyako ndio anakwambia tutachimba hapa mpaka kuleeee na madini yenu yako hapa na pale na utapata dola kadhaa.
Huwezi kupona kuibiwa!
Nimepata fursa ya kufanya kazi na regulatory bodies za nchi kubwa. There is nothing, I mean, I am talking about nothing, ambacho utakuta eti kampuni fulani au mwanasayansi atakuwa anajua kitu fulani kuliko hiyo regulatory body. Heeeell no!!
Na hapo ndio tuna tatizo kubwa nchini. Hizi STAMICO, TCRA, EWURA, TFDA, TANROADS n.k. zinazidiwa utaalam na kampuni zinazozi regulate.
Ndo maana Nyerere akasema jamani eeh we don't know what we are looking at. Tunatembea juu ya madini na hatujijui. Sasa tunafunga haya ma migodi mpaka tutakapojua what we are looking at. Sasa miaka imekwenda imerudi lakini inaonekana bado sana masikini ya Mungu. Mzungu lazima aje atuambie what we are looking at. Inauma mpaka inataka kupasua kichwa.
Tufanyeje kujenga uwezo?