Utajiri wa kishirikina unavyotesa wengi

Utajiri wa kishirikina unavyotesa wengi

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,435
Reaction score
829,792
Utajiri ni ile hali ya kumiliki mapesa mengi na kuwa na mali nyingi, utajiri ni mzuri kwa kuwa unakupa uwezo, nguvu, mamlaka, sifa na umaarufu! Kwa kifupi Utajiri ni kitu chema.

Watu wengi hutafuta utajiri kwa njia mbalimbali halali na haramu wao wanachotaka ni utajiri ili waweze kutimiza ndoto zao nyingi.

Sasa kuna wakati mtu hutafuta utajiri kwa njia za mkato hapa nazungumzia kwa njia za ushirikina na uchawi.

Utajiri huu ni mzuri na huja haraka lakini ukiwa na masharti mengi lakini kubwa likiwa ni kutoa kafara la damu kwa kuangamiza roho.

Unapoingia kwenye utajiri huu mwanzoni utafurahia na masharti utayaona mepesi lakini kadiri siku zinavyozidi kwenda mambo hubadilika na tabu huanzia hapo.

Mwanzoni utaambiwa toa kafara la damu ya kuku baadae itakuja mbuzi, halafu itafuatia ng'ombe na mwishowe itakuja binadamu mmoja na hatimaye kwa makundi.

Hii yote ni kutaka kulinda utajiri wako usiporomoke na ukivunja masharti kila kitu kinaharibika .

Kuna pia masharti ya kujisaidia, kulala, kula, kuvaa na hata matumizi ya vitu mbalimbali. Mwanzoni inakuwa ni rahisi tu kwenda sambamba nayo lakini mbeleni mambo hubadilika hasa pale watu wanapoanza kuhoji hiki au kile.

Wote tunajua jamii ya watu wenye ulemavu wa ngozi inavyoteketea kutokana na waganga wa kienyeji kuwaaminisha wateja wao kuwa viungo hivyo vikichanganywa na dawa nyingine huleta utajiri, bahati, nguvu na uwezo! Kuna zaidi ya waganga 300 kwenye mahabusu na Magereza mbalimbali wenye kesi zinazowahusisha na mauaji ya albino.

Jamani utajiri wa masharti ya namna hii haufai na mwishowe huwa na anguko kuu tunashuhudia visa vya kila aina kuhusiana na utajiri wa namna hii lakini kila uchao watu hawakomi kuendelea kuutafuta.

Hakika dunia inaumwa
 
sitaki hayo mambo ya kwenda kwa mganga kuna jamaa yuko uku mwanza ana ela ila mguu mmoja ni mnene alafu una madonda makubwa yani dah inasikitisha...na ukiona mtu anaenda kwa mganga ujue kwaishiwa maarifa kichwani...

Masharti mengi yanachukiza kwa kweli na ukishakubali kujitia hicho kitanzi huchomoki
 
mshana jr

Bonge moja la topic. Me mtaani kwetu kuna jamaa mmoja basi ameua ndugu zake wote (sacrifice) na juzi juzi mwezi wa pili kammalizia maza ake, at the first sikuelewa coz umri ulikuwa haujachanganua mambo wakati napewa hizi story!

Miaka minne iliyopita na sasa hivi ndo nikaelewa kinachoongelewa, yaani kila akiua anaandika jina mali ( mfano akinunua fuso anaandika jina la ndugu yake aliyekufa) maza ake kafa juzi amenunua mjengo wenye ghorofa mbili kauandika jina la mama ake!

Masharti nuksi!
 
Inawahusu hasa wale wenzetu wa kutoka wilaya ya Makete. Yaani Wakinga. Full mazingaombwe

boss hiyo ni imani yako tu.
wakinga wanatafuta hela mahali popote na wanaishi maisha ya kujibana ndio maana wanakuwa na mali pale wanapozipata.
matumizi mabaya ya kile kidogo unachopata yanakufanya usifanikiwe hata kidogo.

mkinga asubuhi anakunywa chai nyumbani, mchana analetewa chakula kutoka nyumbani, jioni anaenda kula nyumbani kwa nini asiwe na hela?
dukani kwake yupo yeye na mkewe ndio wauzaji akiweka msaidizi basi ni ndugu yake.
kwani wangapi wameenda kwa waganga na bado biashara zikagoma/kuanguka?
siku zote hata kwa anayetegemea mshahara, matumizi mazuri ya anachopata ndio mafanikio yake.
sio mtu kila siku asubuhi anaamkia supu ya kuku, mchana nyama choma na jioni kitimoto na bia juu.
huyu hawezi kufanikiwa.
 
Utajiri una madaraja na kila daraja lina kafara lake mfano
Milioni 20-50 ni tofauti na milioni 100-200 na kila daraja huhitaji kitu kikubwa zaidi au damu nyingi zaidi
 
The sad part is this, when these people die, they all go to hell. Why can't you ask God to bless you?

Proverbs 10: 22 The blessing of the LORD, it maketh rich, and he addeth no sorrow with it.

I love you Jesus.

 
Bonge moja la topic. Me mtaan kwe2 kuna jamaa mmoja mmeru bac ameua ndugu zake wote (sacrifice) na juzi juzi mwezi wa pili kammalizia maza ake, at the first ckuelewa coz umri ulikuwa haujachanganua mambo wakat napewa hizi story! Miaka minne iliyopita na sasa hivi ndo nikaelewa kinachoongelewa, yaan kila akiuwa anaandika jina mali ( mfano akinunua fuso anaandika jina la ndugu yake aliyekufa) maza ake kafa juzi amenunua mjengo wenye ghorofa mbili kauandika jina la mama ake! Masharti nuksi!

Huu ujinga ndiyo unafanya muendelee kuwa maskini..we endelea kuimba masharti masharti wenzako wanatoboa!!
 
Utajiri una madaraja na kila daraja lina kafara lake mfano
Milioni 20-50 ni tofauti na milioni 100-200 na kila daraja huhitaji kitu kikubwa zaidi au damu nyingi zaidi

acha kulisha watu ujinga wewe!!
 
Hata hili wimbi la kupotea kwa watoto lina uhusiano mkubwa na hawa watafuta madaraka hasa kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu

Hata ajili nyingi kutokea ndani ya mwezi mmoja, bila sababu ya msingi kama vile mvua au kuongezeka kwa wasafiri mwezi ule wa pili ni kiashirio kizuri sana kwamba mambo hayo yalipangwa na mawakala wa kifo
 
boss hiyo ni imani yako tu.
wakinga wanatafuta hela mahali popote na wanaishi maisha ya kujibana ndio maana wanakuwa na mali pale wanapozipata.
matumizi mabaya ya kile kidogo unachopata yanakufanya usifanikiwe hata kidogo.

mkinga asubuhi anakunywa chai nyumbani, mchana analetewa chakula kutoka nyumbani, jioni anaenda kula nyumbani kwa nini asiwe na hela?
dukani kwake yupo yeye na mkewe ndio wauzaji akiweka msaidizi basi ni ndugu yake.
kwani wangapi wameenda kwa waganga na bado biashara zikagoma/kuanguka?
siku zote hata kwa anayetegemea mshahara, matumizi mazuri ya anachopata ndio mafanikio yake.
sio mtu kila siku asubuhi anaamkia supu ya kuku, mchana nyama choma na jioni kitimoto na bia juu.
huyu hawezi kufanikiwa.
Ukisikia paa ujue kuna mtu limempata. nina hakika hii post ya Mshana imekushika pabaya
 
Back
Top Bottom